Baada ya jana serikali kupitia Wizara ya
Habari kutoa agizo la kumfungia Snura kutojihusisha na shughuli za
muziki kutoka wimbo wake na kutojisajili Baraza la Sanaa Taifa (BASATA),
leo mwanamuziki huyo na meneja wake HK wameomba radhi kwa umma katika
Ukumbi wa Habari Maelezo, jijini Dar.
n Dawa inayotumika kwa matibabu ya kawaida huenda ikategua kitendawili cha kurefusha maisha na kuzuia uzee. Hii
ni kwa mujibu wa utafiti mpya, ambao ulibainisha kwamba viwango vya
chini vya dawa aina ya Lithium vilisaidia kurefusha maisha ya nzi
waliowekwa kwenye
Rapa Nicki Minaj amefikia wakati mgumu kwenye maisha yake kwenye
kuchagua kuwasiliana na hasimu wa mpenzi wake ambaye ni Drake au kukata
mawasiliano naye kabisa ili kumfurahisha Meek Mill ambaye ni boy friend
wake.
Kwa mujibu wa Hollywood Life Nicki Minaj amemchagua Meek Mill na amekata
mawasiliano kabisa na rapa Drake ambaye wapo pamoja kwenye lebel moja
ya Young Money.
Wawili hawana mawasiliano toka June 2015 beef kati ya Meek na Drake
lilipoanza. Pia mpaka sasa
SWAXBZ
Mtangazaji
wa Clouds FM, Diva amesema nyimbo zake pamoja na za mtangazaji
mwenzake, Adam Mchomvu zinabaniwa na redio zingine, kitu ambacho anaona
si sawa.
Anasema redio za mikoani ndizo zimekuwa zikiwapa support bila kujali
kuwa wanatoka Clouds lakini redio karibu zote za Dar zimekuwa zikibania
nyimbo zao.
Diva ambaye anaandaa album yake, The Life of The Diva, amesema kuwa hicho ni kitu ambacho angependa kuona kinafutika.
Mamaake aliyekuwa mwanamuziki wa mtindo wa Rap Tupac Shakur ,Afeni Shakur amefariki akiwa na umri wa miaka 69.
Kaunti ya California imethibitisha kifo chake kupitia ujumbe wa Twitter.Hakuna maelezo zaidi yaliotolewa.
Alice
Faye Williams,alibadilisha jina lake na kuitwa Shakur akiwa mtu mzima
alipokuwa mwanaharakati wa kisiasa na kujiunga na vuguvugu la Black
Panther.
Alikuwa na mimba ya Tupac mwaka 1971 alipokamatwa na
kufungwa jela pamoja na wanachama
Uzinduzi wa basi la wanawake pekee
katika mji mmoja wa China umewakasirisha wanaume wa taifa hilo na kuzua
mjadala mkali katika mitandao ya kijamii.
Huduma hiyo mpya
itatolewa wakati wa asubuhi na wakati wa shughuli nyingi katika mji wa
mashariki wa Zhengzhou katika juhudi za kupunguza visa vya wanawake
kusumbuliwa na wanaume kulingana na gazeti la Dahe daily.
Kampuni
hiyo ya basi itawalinda wanawake dhidi ya kunyanyaswa wakati wanapovaa
nguo nyepesi
Maelfu ya waombolezaji walijitokeza
kuadhimisha misa ya wafu kwa heshima ya mwanamuziki nyota wa muziki wa
Soukus na Rhumba raia wa Jamhuri ya Congo Papa Wemba.
Waomboloezaji
walipiga foleni ilikupata fursa ya kutoa heshima zao za mwisho kwa
msanii huyo nguli aliyeaga dunia juma lililopita alipokuwa akiwatumbuiza
mashabiki wake huko Abidjan Ivory Coast.
Mwili wake umewekwa katika majengo ya bunge mjini Kinshasa.
Hakimu mmoja nchini Brazili amefunga
mawasiliano ya mtandano wa simu kwa njia ya whatsapp kwa saa 72.Hakimu
huyo Marcel Montalvao amesema kampuni inayomiliki mtandao huo imeshindwa
kusaidia kutoa taarifa katika kesi ya uhalifu.
Mwezi
Machi,Montalvao aliamuru kukamatwa kwa afisa mwandamizi wa Facebook
katika nchi za Kilatini bwana Diego Dzoran baada ya kukataa kutoa
ushirikiano katika uchunguzi dhidi ya dawa za
Wakati ngoma za ‘Bado’ ya Harmonize ft Diamond inaendelea kufanya vizuri na ‘Kwetu’ ya Raymond inaendelea kufanya vizuri, leo Mei 2 2016 Harmonize na Raymondwameingia kwenye headlines baada ya ngoma yao waliofanya pamoja ya ‘Penzi’ kuvuja, millardayo.com imeinasa na kukusogezea track hiyo
LAYIII Watafiti wa University of Pittsburgh School of Medicine walifanya
utafiti kuhusu madhara ya matumizi ya mitandao ya kijamii katika mood
ya watumiaji.
Utafiti huo ulibaini kuwa kadri vijana wanavyotumia mitandao hiyo zaidi,
ndivyo wanavyopata tatizo la sonona ambalo kitaalam linajulikana kama
depression, au kukosa uchangamfu na furaha.
“Kwasababu mitandao ya kijamii imekuwa kitu kilichojiweka kwenye
mawasiliano ya binadamu, ni muhimu kwa wauguzi kuongea na vijana kuhusu
kutambua uwiano unaotakiwa kuwepo na kuhimiza matumizi chanya wakati
wakijiondoa kwenye matumizi yenye matatizo,” alisema Brian A. Primack,
M.D., Ph.D., ambaye ni mwandishi mkuu wa utafiti huo.
L
Mtayarishaji mkongwe wa muziki hapa Tanzania, Master J amesema kuwa
maproducer ndio wanaomiliki beat ila wanawafanyia fair wasanii.
Master J ambaye ni mmiliki wa studio ya MJ Record amefanikiwa kufanya
kazi na wasanii wakongwe wakubwa kwenye muziki wa Bongo Flava lakini pia
alistaafu kazi hiyo ya kuandaa muziki tangu mwaka 2005 na kumuachia
Marco Chali akifanya kazi hiyo.
Akiongea kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Master J
alisema, ‘Maproducer
Mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy ametawazwa mchezaji soka bora wa mwaka na chama cha waandishi wa kandanda Uingereza.
Mshambuliaji
huyo wa Uingereza alipata 36% ya kura zilizopigwa na wanahabari 290 na
kuwashinda wenzake Riyad Mahrez na N'Golo Kante.
Vardy, 29, amefunga mabao 22 Ligi ya Premia msimu huu.
Aidha, alivunja rekodi kwa kufunga mabao kila mechi katika mechi 11 mtawalia.
Meneja wa Arsenal Arsene Wenger
amesema alitarajia mashabiki zaidi waonyeshe kutoridhishwa naye wakati
wa mechi ya Jumamosi dhidi ya Norwich.
Arsenal walishinda 1-0.
Wenger
atatimiza 20 kwenye usukani Arsenal Oktoba mwaka huu lakini mara yake
ya mwisho kushinda ligi ilikuwa 2004 na baadhi ya mashabiki waliinua
mabako ya kusema “wakati wa mabadiliko umefika” uwanjani Emirates.
Shirika la Ujasusi la Marekani (CIA)
limeshutumiwa mtandaoni kwa kusimulia moja kwa moja matukio
yaliyopelekea kuuawa kwa Osama Bin Laden.
Shirika hilo limekuwa
likiandika ujumbe kwenye Twitter na kusimulia matukio yaliyopelekea
kuuawa kwa kiongozi huyo wa mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda kana kwamba
yalikuwa yanafanyika
Watu zaidi ya 45 wamefariki kutokana
na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu visiwani Zanzibar katika kipindi
cha miezi miwili, shirika la habari la AP limeripoti.
Shirika hilo la habari limemnukuu afisa wa afya visiwani humo anayesema vifo hivyo vimetokea mwezi Machin a Aprili.
Muhammed
Dahoma, ambaye ni mkurugenzi wa anayeangazia kuzuia maradhi katika
wizara ya afya, anasema watu karibu 3,000 wamelazwa hospitalini baada ya
kuugua.
Ameongeza kuwa serikali ya Zanzibar imechukua hatua kukabiliana na mlipuko huo.
Miongoni mwa hatua zilizochukuliwa ni kupiga marufuku uuzaji wa chakula na juisi maeneo ya wazi.
Taarifa kutoka visiwani humo zinasema serikali pia imeamuru kufungwa kwa shule zote kwa muda usiojulikana.
Waziri
wa elimu Riziki Pembe Juma, amenukuliwa na shirika la habari la Uchina
la Xinhua, akisema uamuzi huo umetolewa baada ya kubainika kwamba
wanafunzi ni miongoni mwa watu walioathiriwa zaidi na ugonjwa huo.
“Tumejaribu
kudhibiti hali, lakini kwa maslahi ya watoto wetu, watakuwa salama
zaidi wakisalia nyumbani,” amesema kupitia taarifa, kwa mujibu wa
Xinhua.
Ameongeza kuwa baadhi ya shule zimeathirika zaidi kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na mvua kubwa inayoendelea kunyesha.
Kisiwa cha Unguja ndicho kilichoathirika zaidi ambapo watu 20 wamefariki na 400 kuambukiwa tangu Januari mwaka huu.
Waziri
wa afya Mahmoud Thabit Kombo aliambia gazeti la serikali la Daily News
wiki jana kwamba ikizingatiwa kwamba Zanzibar ni visiwa vidogo na watu
si wengi sana “kipindupindu sasa ni tishio kubwa”.
Mlipuko wa kipindupindu ulianza mwaka jana.
Kufikia Oktoba, visa 140 vya maambukizi vilikuwa vimeripotiwa katika visiwa hivyo kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO).
Miili ya wakwea milima wawili kutoka Marekani waliotoweka katika milima ya Himalaya miaka 16 iliyopita imepatikana.
Mkwea
milima maarufu duniani Alex Lowe alikuwa akikwea katika kilele cha
Shishapangma chenye urefu wa 8,013m (26,290ft) eneo la Tibet Oktoba 1999
akiwa na mpiga picha David Bridges mkasa ulipotokea.
Wawili hao walifukiwa na maporomoko ya theluji.