SWAXBZ
Baada ya jana serikali kupitia Wizara ya
Habari kutoa agizo la kumfungia Snura kutojihusisha na shughuli za
muziki kutoka wimbo wake na kutojisajili Baraza la Sanaa Taifa (BASATA),
leo mwanamuziki huyo na meneja wake HK wameomba radhi kwa umma katika
Ukumbi wa Habari Maelezo, jijini Dar.
“Tumewaita Waandishi wa habari kwa ajili
ya kuomba radhi kwa Umma na Watanzania kwa ujumla kwa kisa la
kutengeneza, kuzindua na kuweka mtandaoni video ya udhali…lishaji wa Mwanamke na isiyozingatia maadili ya Kitanzania ya muziki unaoitwa “Chura”.
Tunaviomba radhi vyombo vya Serikali
vinavyosimamia sekta ya Sanaa kwa kutofuata sheria, kanuni na taratibu
zilizopo katika uendeshaji Sanaa nchini, mimi na meneja tunaahidi
kutorudia tena kufanya tukio hilo la udhalilishaji, na iwapo tutarudia
basi tupewe adhabu kali kwa mujibu wa sheria za nchi hii.” Snura
No comments:
Post a Comment