Monday, 2 May 2016

VARDY MCHEZAJI BORA WA MWAKA UINGEREZA

LAYIII
Vardy
Mshambuliaji wa Leicester Jamie Vardy ametawazwa mchezaji soka bora wa mwaka na chama cha waandishi wa kandanda Uingereza.
Mshambuliaji huyo wa Uingereza alipata 36% ya kura zilizopigwa na wanahabari 290 na kuwashinda wenzake Riyad Mahrez na N'Golo Kante.
Vardy, 29, amefunga mabao 22 Ligi ya Premia msimu huu.
Aidha, alivunja rekodi kwa kufunga mabao kila mechi katika mechi 11 mtawalia.

Klabu yake inahitaji alama mbili pekee kushinda Ligi Kuu ya Uingereza lakini inaweza pia kutawazwa mabingwa iwapo Tottenham watashindwa kuwalaza Chelsea jioni.
Mahrez alishinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka ya PFA, ambayo mshindi hupigiwa kura na wachezaji soka ya kulipwa, mwezi jana.


No comments:

Post a Comment

advertise here