Monday, 2 May 2016

Utafiti: Matumizi makubwa ya mitandao ya kijamii yanasababisha sonona (depression)

LAYIII

Watafiti wa University of Pittsburgh School of Medicine walifanya utafiti kuhusu madhara ya matumizi ya mitandao ya kijamii katika mood ya watumiaji.

Utafiti huo ulibaini kuwa kadri vijana wanavyotumia mitandao hiyo zaidi, ndivyo wanavyopata tatizo la sonona ambalo kitaalam linajulikana kama depression, au kukosa uchangamfu na furaha.

“Kwasababu mitandao ya kijamii imekuwa kitu kilichojiweka kwenye mawasiliano ya binadamu, ni muhimu kwa wauguzi kuongea na vijana kuhusu kutambua uwiano unaotakiwa kuwepo na kuhimiza matumizi chanya wakati wakijiondoa kwenye matumizi yenye matatizo,” alisema Brian A. Primack, M.D., Ph.D., ambaye ni mwandishi mkuu wa utafiti huo.


Utafiti huo ulihusisha watu 1,787 nchini Marekani wa kuanzia miaka 19 hadi 32. Mitandao iliyohusishwa ni pamoja na Facebook, YouTube, Twitter, Google Plus, Instagram, Snapchat, Reddit, Tumblr, Pinterest, Vine na LinkedIn.

Washiriki walitumia mitandao hiyo kwa dakika 61 na kutembelea akaunti mbalimbali za mitandao ya kijamii mara 30 kwa wiki, kiwastani. Cha kutisha kwenye utafiti huo, zaidi ya robo ya washiriki walielezewa kuwa na viashirio vya juu vya sonona.

Kulikuwepo na uhusiano mkubwa kati ya matumizi ya mitandao ya kijamii na sonona.

Watafiti hao lakini walizitaja sababu zingine zinazochangia tatizo hilo kuwa ni pamoja na umri, jinsia, rangi, uhusiano, hali ya maisha, kiwango cha elimu na kipato. 


No comments:

Post a Comment

advertise here