Monday, 2 May 2016

WASANII WANAFANYIWA FAIR SANA :MANENO YA MASTER J

LAYIII

L
Mtayarishaji mkongwe wa muziki hapa Tanzania, Master J amesema kuwa maproducer ndio wanaomiliki beat ila wanawafanyia fair wasanii.

Master J ambaye ni mmiliki wa studio ya MJ Record amefanikiwa kufanya kazi na wasanii wakongwe wakubwa kwenye muziki wa Bongo Flava lakini pia alistaafu kazi hiyo ya kuandaa muziki tangu mwaka 2005 na kumuachia Marco Chali akifanya kazi hiyo.

Akiongea kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Master J alisema, ‘Maproducer
wanawafanyia fair wasanii lakini beat ni mali zao.’

“Sheria zipo ila kihali ya ubinaadamu maproducer wanafanya fair tu, wakilipwa hela ya kutemtengenezea wimbo msanii ndio imetoka. Lakini sheria zipo wazi tu, mimi niliandaa albamu ya Sugu yenye nyimbo kumi na kila wimbo alinilipa elfu kumi tu,kwahiyo kwa elfu kumi nikamuachia kila kitu,” aliongezea.

Aidha Master J amemsifu Lucci kwa uamuzi wake wa kuingia kwenye utengenezaji wa matangazo ambao ndiyo unalipa zaidi kuliko malipo wanayoyapata maproducer kwa wasanii. 



No comments:

Post a Comment

advertise here