Vidonda vya tumbo kwa mama mjamzito
Mwanamke mjamzito anaweza kupata vidonda vya tumbo kabla au baada ya ujauzito. Hata hivyo tafiti nyingi zinathibitisha idadi ya wanawake wajawazito wanaopatwa na vidonda vya tumbo kwa sasa ni ndogo sana.
Umakini unahitajika sana katika kumchunguza mama mjamzito ili kuelewa nini kitakuwa ndiyo chanzo cha vidonda vya tumbo kwake.
Mwanamke ambaye ulikuwa unaumwa vidonda vya tumbo hata kabla ya kushika ujauzito unaweza kuendelea kutumia baadhi ya dawa rafiki (hasa zitokanazo na vyakula na mimea) za kutibu au kuzuia dalili za