Tuesday 29 March 2016

NICK MINAJ AWAKA KWA HASIRA DHIDI YA MLINZI WAKE

LAYIII
MSIKILIZE HAPPYNESS HAPA BONYEZA PICHA YA NICK MINAJI
Hii ishu imetokea wakati Nicki Minaj akifanya show Dubai na kilichotokea ni kwamba Mlinzi wake huyo hakuwa makini na kazi, wakati Nicki yuko kwenye stage anaimba, akagundua kwamba upande wake wa kulia mmoja wa Walinzi wake hafanyi kazi inavyotakiwa maana kashika simu yake ya mkononi.

Nicki alichofanya ni kwenda kumnyang’anya ile simu alafu akaitupa nyuma ya stage kwenye upande ambao watu wake wengine walikuwepo na haikujulikana kama Nicki Minaj aliongea chochote baada ya show kumalizika ila media zimeripoti kukasirika kwake na kushindwa kujizuia kama inavyoonekana kwenye hii video hapa chini.
Kitendo cha Nicki kutupa hiyo simu kimepokelewa tofauti, kuna wengine wamesema ni sawa sababu amemlipa yule jamaa kwa ajili ya kumlinda na sio kushika simu wakati wa kazi, wengine wamesema Nicki ameonyesha ni kiasi gani hana adabu kwa sababu angeweza kuvumilia hiyo ikapita.
nicki 2nicki 1

No comments:

Post a Comment

advertise here