Wednesday 20 April 2016

MVUA YAONGEZA MAJI MACHAFU BWAWA LA KIDATU HOFU YA KUHARIBIKA KWA MIUNDO MBINU YATANDA

LAYIII
Bonyeza picha hii hushuhudia volcano ilivyowaka ndani ya bwawa flani maeneo ya iringa
https://youtu.be/8B2S3rtS304
Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha kuongezeka kwa maji kupita kiasi katika bwawa la kufua umeme la Kidatu na kuvuka kiwango chake cha kawaida cha mita za ujazo 450 hadi 450.5 kutoka usawa wa bahari, hali inayotishia kuharibika kwa miundo mbinu ya bwawa hilo na maji kuwaathiri wananchi wanaofanya shughuli zao zikiwemo za uvuvi na kilimo kandokando ya mto Ruaha mkuu na Kilombero.
Mkurugenzi mkuu wa shirika la umeme Tanzania Tanesco Mhandisi  Felchecim Mramba amesema maji hayo yakiachiwa, yanaweza kusababisha maafa makubwa na hasara kubwa kwa taifa, kwani miundo mbinu itaharibika na uzalishaji wa umeme hautaweza kuendelea, wakati umeme unaotumia maji umekuwa na
manufaa makubwa ikilinganishwa na ule unaotumia nishati nyingine na mara ya mwisho hali kama hiyo kujitokeza ilikuwa ni mwaka 2007.
Kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa ikiongozwa na mkuu wa mkoa wa Morogoro Dk Kebwe Steven Kebwe na uongozi wa Tanesco wamelazimika kutembelea maeneo hayo na kuamuru kufunguliwa kwa mageti makubwa yaliyojengwa maalum kudhibiti maji, ambayo maji kwa sasa yanalazimika kupita juu yake, jambo ambalo sio salama kitaalamu, huku wananchi wakitakiwa kuchukua tahadhari hasa wakati huu mvua zinapoendelea kunyesha na mkoa wa Morogoro ukiwa ni miongoni mwa mikoa 10 iliyotajwa kupata mvua za juu ya wastani. 
Bwawa hilo mwaka jana lilikuwa na maji chini ya mita 433 kutoka usawa wa bahari, kiwango ambacho ni cha chini sana, huku mwaka huu ikielezwa wingi huo wa maji umetokana na maji ya mto Lukosi na Iyovi ya Morogoro pekee huku yale yanayotoka bwawa la Mtera yakiwa yamezuiliwa kwa sasa.


No comments:

Post a Comment

advertise here