Wednesday 20 April 2016

ALIENS WAITAJIRISHA MAREKANI

BONYEZA PICHA KUJIUNGA NAMI YOUTUBEhttps://www.youtube.com/watch?v=g2KepoPu_C0Wiki iliyopita nilianza simulizi hii ya viumbe wa ajabu waitwao Aliens waishio angani. Niliishia pale nilipoanza kueleza ni viumbe gani hawa ambao wamekuwa wakihusishwa na upotevu wa watu na ndege duniani? SASA ENDELEA…
Juu ya viumbe hawa wa ajabu waishio angani waitwao Aliens, mifano mingi inayotolewa inalenga kuthibitisha kuwa kweli kuna viumbe wa ajabu ambao wamekuwa wakishindana na binadamu bila wenyewe kujua hivyo kuwapa kazi kubwa wanasayansi wa anga kufanya utafiti wa ziada.



Katika simulizi hii inaweza kuniwia vigumu kuthibitisha au kukiri kuwa naamini uwepo wa viumbe hawa ila ninachojaribu kukifanya ni kukutengenezea mazingira kuwa mbali na majini na mashetani, angani kuna viumbe, bakteria, vitu na hata virusi ambavyo bado wanasayansi duniani hawajavigundua.
Kumbuka; si kila kilichopo mtandaoni ni cha kweli. Hata wewe unaweza kubuni simulizi za aina fulani na ukapata wafuasi wa kutosha. Kidogo tu nithibitishe hilo kisha tuendelee na simulizi yetu. Kuhusu familia za kitajiri au kifalme kumekuwa na stori kuwa hubadilika na kuwa reptilia. Hizo ni stori tu na zipo nyingi ambapo hakuna uthibitisho kwa kuonekana ni uchawi au mambo ya kishetani.
Kuna baadhi ya binadamu wanaoamini uwepo wa Aliens hasa baada ya kutazama filamu nyingi za Kimarekani zilizobeba simulizi za viumbe hawa. Kama ulifanikiwa kufuatilia Runinga ya ITV ya Tanzania, miaka kadhaa iliyopita, kuna ‘series’ ya tamthiliya ilikuwa ikirushwa ya Babylon 5 iliyokuwa ikionesha maisha yanavyoendelea huko angani kuhusu hawa Aliens.
Pia ipo sinema nyingine ya Kihindi ambayo inawahusu Aliens inayoitwa Koi Milgaya au I Found Someone, nayo inathibitisha uwepo wa hawa viumbe duniani japokuwa wapo wanaomini ni mambo ya kusadikika tu.
Kuna uthibitisho kwamba series za hawa Aliens, Vampires, Super Heroes, Golins, Ware Wolves na zingine nyingi, ni kati ya vitu vinavyopendwa kufuatiliwa na binadamu hasa kabla ya kulala kwa kuwa zinaonesha maisha nje ya ulimwengu wa kawaida.
Mapitio ya baadhi ya wanasayansi yanaonesha kuwa mbali na Aliens hakuna kiumbe kingine kilichogundulika nje ya sayari ya dunia. Kilichobaki ni makisio kuwa huenda sayari zingine kuna uwezekano wa kuwepo na uhai kulingana na hali ya hewa na dalili ya uwepo wa maji ingawa bado haijathibitishwa 100%, mfano Mars.
Kama nilivyoeleza awali kuwa kuna sinema nyingi tunazoziona kuhusu hawa Aliens ni maendeleo tu ya kisayansi ndiyo maana Hollywood, Marekani wamepiga fedha na utajiri mkubwa huku mambo mengi yakiwa ni simulizi za kufikirika.
Kuna watu wanaamini kuwa kila wanachosema Wamarekani katika sayansi ni kweli. Si kweli. Ikumbukwe kuwa vitu visivyojulikana angani (UFO) siyo viumbe na si kweli kwamba Wamarekani hawajui vile ni vitu gani.
Inaaminika kuwa UFO (Unidentified Flying Object) ni matokeo ya maendeleo ya sayansi ya anga kati ya wanasayansi wa Kimarekani na hawa Aliens na Wamarekani wanaujua ukweli juu ya jambo hilo.
Habari nyuma ya pazia ni kwamba wanasayansi wa Kimarekani hawataki kabisa wanadamu wa kawaida wajue uhusiano wao na hawa Aliens kwa sababu inaaminika ni mambo ya kishetani! Katika moja ya ripoti zao kupitia Shirika la Utafiti wa Anga ya Juu la Marekani (NASA), wanasayansi hao waliwahi kuripoti kwamba kwenye moja ya safari zao angani walipokuwa wanakwenda kutua mwezini, njiani waliona chombo chenye viumbe hao wa ajabu wa Aliens.

No comments:

Post a Comment

advertise here