Wednesday, 20 April 2016

MAUMIVU YA TUMBO

LAYIII
JIUNGE NA BZTV BONYEZA PICHA HAPA

Maumivu ya tumbo ni dalili inayosumbua watu wengi kwa wakati na umri tofauti. Karibu kila mtu katika maisha yake atapata namna fulani ya maumivu ya tumbo. Kuna sababu mbalimbali zinazosababisha maumivu ya tumbo na mara nyingi huwa sio za kutisha, hutubiwa na kupona. Mara chache husababishwa na hali ambazo zinaweza kuhatarisha maisha yako. Maumivu yanaweza kuwa katika sehemu maalum ya tumbo au tumbo zima.


Maumivu Ya Tumbo
Ni vizuri ukijua aina ya maumivu ya tumbo unayopata pamoja na dalili zinazoambatana nayo. Hii itasaidia kujua sababu ya maumivu na katika matibabu. Maumivu ya tumbo yanaweza kuwa maumivu ya kuchoma, kuungua, kukandamiza, kukata au. Yanaweza kuwa yanakuja na kuacha baada ya muda fulani. Pia yanaweza kuambata na dalili nyingine kama kutapika, kuharisha, kukosa choo, kupata choo chenye damu, tumbo kuvimba na homa.

Sababu za Maumivu ya Tumbo
Kuna hali nyingi zinazoweza kusababisha maumivu ya tumbo. Chanzo cha maumivu hutegemea na sehemu maumivu yalipo.

Maumivu chini ya mbavu kulia yanaweza kusababishwa na
• Mawe kwenye mfuko wa nyongo
• Maambukizi kwenye mfuko wa nyongo (cholecystitis)
• Uvimbe wa ini
• Jipu kwenye ini
• Homa ya ini
• Saratani ya kongosho na kifuko cha nyongo.

Maumivu chini ya chembe ya moyo
• Vidonda vya tumbo
• Kiungulia
• Saratani ya tumbo
• Saratani ya kongosho

Maumivu Pembeni mwa kitovu
• Mawe ya figo (kidney stones)
• Maambukizi ya figo (pyelonephritis)
• Maambukizi kidoletumbo (Acute appendicitis)

Maumivu chini ya kitovu
• Maambukizi ya mfumo wa mkojo
• Magonjwa ya zinaa kama klamidia, PID
• Vivimbe vya mji wa uzazi
• Mimba kuharibika
• Saratani ya kibofu cha mkojo
• Premenstrual Syndrome – PMS

Sababu nyingine za maumivu ya tumbo ni;
• Irritable bowel syndrome
• Utumbo kujiziba (intestinal obstruction)
• Utumbo kujisokota (volvulus)
• Food poisoning
• Allergy ya chakula
• Ugonjwa wa Crohn (Crohn’s disease)
• Ngiri (hernia)
• Homa ya tumbo (typhoid fever)

Kama unapta maumivu makali sana ya tumbo, yanajirudia au yanambatana na dalili zozote kati ya zifuatazo basi onana na daktari mapema iwezekanavyo.
• Homa
• Kutapika matapishi yenye damu
• Kutapika sana
• Kukosa choo hasa ikiambatana na kutapika
• Tumbo kuvimba
• Kama umeumia

Matibabu
Maumivu ya tumbo hutibiwa kutokana na sababu ya maumivu. Wakati ukielekea hospitali kwa ajili ya matibabu unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu kama paracetamol au diclofenac.

Ukifika hospitali mtaalamu wa afya atachukua historia ya ugonjwa wako na kisha kufanya uchunguzi pamoja na vipimo vitakavyokuwa muhimu kutokana na aina ya maumivu unayopata.

Kuna njia mbalimbali za matibabu za matatizo yanayosababisha maumivu ya tumbo, ikijumuisha dawa za kunywa au kuchoma na upasuaji.

No comments:

Post a Comment

advertise here