Wednesday 20 April 2016

UROJO UMEPIGWA MARUFUKU KUUZWA ZANZIBAR

LAYIII
JIUNGE NA BZTV BONYEZA PICHA HAPA
https://www.youtube.com/watch?v=M3iWPmDcf5g
WIZARA ya Afya ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) imepiga marufuku biashara za vyakula, ikiwemo vya maji maji kama urojo zinazofanywa na wafanyabiashara ndogo pembezoni mwa barabara kutokana na kuongezeka kwa hofu na kasi ya ugonjwa wa kipindupindu.

Waziri wa Afya, Mahmoud Thabit Kombo wakati akitoa taarifa kuhusu ugonjwa wa kipindupindu, amesema hali imekuwa mbaya zaidi katika kipindi hiki cha mvua za masika zinazoendelea kunyesha nchini kote.


Alisema Serikali imeamua kupiga marufuku uuzaji wa bidhaa za vyakula vya maji maji, ikiwa ni hatua mojawapo ya kupambana na ugonjwa huo kwani katika kipindi cha hivi karibuni kutokana na mvua za masika kasi ya ugonjwa huo imekuwa ikiongezeka.

Alizitaja sababu za kuongezeka kwa kasi ya ugonjwa wa kipindupindu ni kuwepo kwa mazingira yasiyoridhisha ya uchafu. Aliyataja baadhi ya maeneo ambayo yanakabiliwa na hali mbaya ya uchafu kutokana na kufurika kwa makaro na maji ya kawaida kuchanganyika na kinyesi ni Sebleni, Jang’ombe, Chumbuni na Fuoni ambapo zaidi ya nyumba 30 zimezingirwa na maji na wakazi wake kulazimika kuzihama nyumba hizo.

Naye Mkurugenzi wa Kinga katika Wizara ya Afya, Dk Mohamed Dahoma akizungumza na waandishi wa habari alisema hali ya ugonjwa wa kipindupindu kasi yake imekuwa ikitisha ambapo kwa upande wa Unguja maambukizi yamefikia asilimia 52 wakati katika kisiwa cha Pemba yakifikia 41.

Alisema tangu ugonjwa huo kuripotiwa katika kisiwa cha Unguja na Pemba Septemba mwaka jana, tayari watu 38 wamefariki dunia huku watu 2,700 wakiambukizwa ambapo zaidi ya nyumba 10,000 zimefanyiwa ukaguzi, ikiwemo zile zilizogundulika kuwepo kwa wagonjwa hao.

JIFUNZE TEKNOLOJIA YA KUHACK KWA DAKIKA CHACHE

No comments:

Post a Comment

advertise here