Tuesday, 29 March 2016

MANENO YA MBEYA CITY BAADA YA TAARIFA KUHUSU JUMA KASEJA KUSAMBAZWA

LAYII

Klabu ya Mbeya City ya jijini Mbeya ambayo inachezewa na golikipa wa zamani wa vilabu vya Simba na Yanga Juma Kaseja, mchana wa March 28 imeamua kuweka taarifa sawa kuhusiana na tetesi au uvumi uliokuwa unasambazwa mtandaoni kuhusuKaseja.

Mbeya City imetumia ukurasa wake wa instagram, baada ya kuzipata taarifa zisizo za kweli kuhusu uvumi kuwa golikipa wao Juma Kaseja amefariki Dunia, ukweli ni kuwa huo ni uzushi uliotungwa na watu, Juma Kaseja ni mzima na leo amefanya mazoezi na timu.
kaseja
Hii ndio post ya Mbeya City iliyotoa ufafanuzi kuhusu tetesi hizo.
“Kuna taarifa zinasambazwa kwenye mitandao ya kijamii hivi sasa kuwa kipa Juma Kaseja amefariki Dunia, tuchukue nafasi hii kuwajulisha kuwa taarifa hizo sio za kweli, Kaseja yupo salama na leo alifanya mazoezi na timu kujiandaa na mchezo dhidi ya Coastal Union”

No comments:

Post a Comment

advertise here