Wednesday 30 March 2016

UKWELI KUHUSU UKIMWI

LAYIII

Ukimwi
Ukimwi

Fuatana nami katika makala hii ndefu, unaweza kuzima kabisa intaneti yako wakati ukiendelea kusoma.
‘’Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa; kwa kuwa wewe umeyakataa maarifa, mimi nami nitakukataa wewe, usiwe kuhani kwangu mimi; kwakuwa umeisahau sheria ya Mungu wako, Mimi nami nitawasahau watoto wako – Hosea 4: 6’’.
Ukweli Kuhusu UKIMWI ni maelezo yanayoipinga dhana inayosema ugonjwa wa UKIMWI husababishwa na Virusi Vya Ukimwi (V.V.U) kupitia maandiko kadhaa ambayo yameshaandikwa na wanasayansi wengine
duniani.
UKIMWI ni nini?
  • Je ni kweli UKIMWI husababishwa na Virusi Vya Ukimwi (V.V.U)?
  • Je ni kweli UKIMWI ni ugonjwa wa kuambukizana?
  • Je ni kweli watu wanapona UKIMWI?
Maelezo haya yanatolewa kama elimu tu kwa umma na si lengo la mwandishi kumuondoa daktari wako au chaguo lako la matibabu unayopendelea, matumizi ya taarifa zilizomo humu yanabaki kuwa jukumu la msomaji, mwandishi wa makala hii hatoi dhamana yeyote juu ya yale yawezayo kutokea katika afya yako kutokana na taarifa au ujuzi utakaoupata toka hapa, badala yake ubadilishanaji wa taarifa na maarifa yaliyomo humu na daktari au jamaa zako wengine unahimizwa sana kwa ustawi wa dunia yetu.
ANGALIZO: Unaruhusiwa kukopi makala hii yote kwa matumizi yako binafsi tu na siyo kwenda kuiweka kama ilivyo kwenye blog yako au mahala pengine popote bila ruhusa.

UKIMWI ni nini?

Neno UKIMWI ni kifupi cha maneno: Upungufu wa Kinga Mwilini. Tumeambiwa ni ugonjwa unaotokana na virusi vya UKIMWI (V.V.U) au Human Immunodeficiency Virus (H.I.V) kwa lugha ya kikoloni.
Tumefundishwa kuwa virusi hao wakiingia katika damu ya binadamu huenda kuishi katikati ya seli na kuzidhuru chembe chembe hai nyeupe za damu ambazo ndizo huhusika na kinga ya mwili na hivyo kumuweka mhusika katika hali ya kupatwa na magonjwa mengi nyemelezi zaidi ya 30 na kuwa hadi sasa hakuna dawa inayoweza kutibu virusi hivyo au kwa maneno mengine UKIMWI hauna dawa!
Tumefundishwa kuwa virusi vya UKIMWI vinaweza kuambukizwa toka kwa mtu mmoja hadi mwingine kwa sehemu KUBWA kupitia tendo la ndoa ambapo damu ya aliyeathirika na virusi hivi ikikutana na ambaye hajaathirika wakati huo wa tendo la ndoa basi virusi navyo humwingia mtu huyo, njia nyingine ni kwa kushirikiana vifaa vyenye ncha kali kama vile nyembe, sindano, mikasi na kadharika, nyingine ni mama mjamzito kumwambukiza mwanaye wakati wa kujifungua au anaponyonyesha, mgonjwa aliyechangiwa damu yenye virusi na kadharika.
Tangu kuanza kutangazwa kwa ugonjwa huu mwanzoni mwa miaka ya 1980 maelfu ya watu wamekufa duniani kote huku mamilioni wengine wakisemwa wanaendelea kuishi kwa matumaini wakitumia dawa za kupunguza makali kundi la ARV’s.
Hivyo ndivyo tulivyofundishwa na kuaminishwa kuhusu UKIMWI.
                                                            
Je ni kweli UKIMWI husababishwa na virusi vya UKIMWI?
Ingawa kwa miaka mingi tumefundishwa kuwa UKIMWI husababishwa na virusi vya ukimwi (v.v.u) ukweli ni kuwa jambo hilo si la kweli na hapa chini tutaona sababu 10 za kisayansi zinazoeleza kwanini virusi vya ukimwi/HIV vilivyo havina uwezo wa kusababisha ukimwi mwilini au hata ugonjwa mwingine wowote.
SABABU 10 ZA KISAYANSI KWANINI HIV/VVU HAVIWEZI KUSABABISHA UKIMWI/AIDS:
“Kile kila mtu anajua na kukiamini” wakati mwingine kinaweza kuwa si cha kweli. Yanapokuja masuala yanayohusiana na sayansi, ikiwa ni pamoja na sayansi ya matibabu, historia inaweza hata kupendekeza kwamba kile kila mtu anajua wakati wowote kinaweza kugeuka baadaye na kuwa siyo sahihi kwa kiwango fulani: ufahamu wa kisayansi umeongezeka, na pamoja na kuendelea huko kwa sayansi, mara nyingi maendeleo hayo yametokea kwa kupindua nadharia zilizotangulia.
Lakini pamoja na kutambua kuwa sayansi imezidi kupaa, huku kila mmoja akiamini hivyo, mara nyingi watu wamesahau kwamba maendeleo hayo yametokana na kukanusha au kupindua nadharia zilizokubalika kabla za kisayansi. Na dhana kwamba nadharia iliyotangulia yaweza kuwa si sahihi, inaweza kuchelewa sana kukubaliwa na watu wengi.
Hivyo madai kwamba Virusi Vya Ukimwi (VVU/HIV) havina uwezo wa kusababisha UKIMWI mwilini, wakati kila mtu anajua kwamba virusi hao husababisha UKimwi, yanachukuliwa na vyombo vya habari, umma, na sayansi tawala kama si vitu vya kuvitilia mkazo. Hata hivyo ushahidi kwamba HIV haiwezi kuwa sababu ya UKIMWI umejitokeza katika maandiko ya kisayansi, na katika dazani kadhaa za vitabu, tovuti na video zikielekezwa kwa sehemu kubwa moja kwa moja kwa umma.
Ni vema kutozingatia kutoa tu ushuhuda kwamba V.V.U havisababishi UKIMWI, bali mhimu iwe kutoa maelezo mhimu na ya kweli mbadala ya kutosha kufafanua UKIMWI (AIDS) ni nini na VVU (HIV) ni nini.
Hivyo majibu ya aya hiyo hapo juu yanatakiwa kuonesha kwanini nadharia inayosema VVU (HIV) = UKIMWI (AIDS) ilivyo si sahihi.
1. VVU/HIV huvunjwavunjwa na kinga ya mwili (antibody immunity):
Wakati mtu amepimwa na kukutwa positive (+) kwa V.V.U, humaanisha mtu huyo anayokinga dhidi ya V.V.U (yaani anao uwezo binafsi wa kuviangamiza virusi, anayo kinga). Hili ni wazi kutokana na ukweli kwamba ni virusi wachache huweza kupatikana katika mwili wa aliyekutwa na kinga positive (+) kwa VVU/HIV *, Kinga ya mwili imefanya kazi yake na virusi wanawekwa vizuri chini ya ulizi na kutafunwa. Hakuna na hakujawahi kutokea virusi wanaojulikana ambao wamewahi kusababisha ugonjwa kwa mtu huku kinga ya mwili ikijitokeza kwa muda mrefu, Bali hivi ndivyo UKIMWI ulivyotafsiriwa!.
Mtu anaweza kujiuliza kwanini zaidi ya miongo mitatu sasa, mabilioni ya fedha yameelekezwa kutafiti chanjo dhidi ya V.V.U wakati chanjo bora tayari ipo wakati mtu anapopima na kukutwa positive (+)?.
2. VVU/HIV huwa haviiui T-Seli yake inayoiambukiza:
V.V.U/H.I.V vinaweza tu kuiua T-Seli yake kwa nadra sana katika majaribio ya kimaabara. Kusema ukweli, watafiti wa V.V.U Hutumia T-Seli ili kukuza virusi sababu T-Seli huishi katika mfanano na V.V.U.
3. V.V.U/H.I.V havina uwezo wa kuzidhuru T-Seli vya kutosha na kusababisha UKIMWI:
V.V.U kamwe hazidhuru T-Seli zaidi ya 1 kati ya T-Seli 1000. Kwa kawaida V.V.U huweza kudhuru T-Seli 1 tu kati ya T-Seli 10,000*, Mwili huzarisha asilimia 5% ya T-Seli zake kwa siku. Hesabu rahisi inaonyesha kuwa V.V.U hawawezi kuzidhuru T-Seli za kutosha na kuzifanya (T-Seli) zife zote mpaka kuishusha chini kinga nzima ya mwili.
Hata wafuasi wa nadharia ya VVU / UKIMWI hukubali kwamba hiki kiwango cha chini cha udhurikaji wa T-Seli kutokana na VVU ni changamoto kwao kuielezea.
4. VVU/HIV hakina Jeni (gene) ya kusababisha UKIMWI:
VVU/HIV hakina gene maalum au sababu ya kipekee ya kusababisha UKIMWI. Retrovirus wote wana jenetiki jeni 3 tu kuu, GAG, ENV na POL na gene zingine ndogo 6 tu. Kwa sababu jeni na utaratibu wa kimfuatano wa kijenitiki katika viumbe hawa rahisi ni mdogo, huhitaji gene zao ili kujirudufu. VVU/HIV hakina tofauti na retrovirusi wengine wote kivinasaba. Kuna retrovirusi 50 hadi 100 tofauti ambao wanaweza kupatikana katika kila mwili wa mtu yeyote mwenye afya. Retrovirusi wote hao 50 mpaka 100 wapo chini ya ulinzi wa kinga ya mwili (antibody). VVU/HIV hakina tabia tofauti yoyote ambayo retrovirusi  wengine hawana. Kama retrovirusi hawa wengine hawawezi kusababisha UKIMWI, kwa nini virusi vya ukimwi/HIV? Na kinyume chake, kama HIV husababisha UKIMWI, kwanini hao wengine 50 mpaka 100 hawasababishi Ukimwi? Hivyo hakuna sababu inayoweza kueleza jenetiki ya VVU iwezavyo kusababisha UKIMWI.
5. Hakuna kitu kimewahi kutokea kinaitwa “kirusi cha polepole”:
VVU/HIV vinadaiwa kuchukua miaka 10 hadi 20, kipindi kinachomchukuwa mtu kutoka alipoambukizwa virusi hadi kuugua Ukimwi. Njia pekee ya kuelezea hili ni kuvipa uwezo VVU wa kiuchawi wa kujiamsha (reactivate), uwezo wa kujibadili (mutate), uwezo wa kuhama (migrate) na uwezo wa kupumbaa (hibernate).
Nadharia hizi za virusi vinavyoshambulia polepole zilibuniwa na wanasayansi waliovitumia kununua muda wakati ambapo virusi wao waliposhindikana kuthibitishwa. Watetezi wa virusi vya polepole wanatumia mifano ya virusi kama wa malengelenge (herpes viruses) ambao huunguza polepole na kujificha na kisha kujitokeza tena katika watu wenye virusi hao wakati kinga zao zinapotikiswa na kuishiwa uwezo wa kutosha kuvidhibiti.
Zoezi hili hutofautiana sana katika VVU kwa sababu kiasi kikubwa sana cha virusi wanaweza kupatikana na kusababisha dalili fulani maalum. Kinyume chake, virusi wa taratibu ni uvumbuzi unaoelekeza uwezo wa virusi kusababisha ugonjwa miaka mingi tu baada ya maambukizi – wanakiita kipindi cha kuishi kwa matumaini – katika watu wenye afya bali wanaishi na VVU, bila kujali hali yao ya kinga. Dhana hii inaruhusu wanasayansi kulaumu virusi vilivyokwisha kuvunjwavunjwa baada ya ugonjwa wowote unaojitokeza miongo kadhaa baada ya kuambukizwa VVU. VVU kilishavunjwavunjwa ulipopima na kukutwa positive (+), lakini bado VVU kinasadikika kusababisha zaidi ya magonjwa 30 tofauti miaka hata 10 baadaye.
Hakuna ugonjwa hata mmoja katika haya magonjwa 30 na zaidi wenye uhusiano maalumu hata na VVU vyenyewe. Kwa kawaida ugonjwa utokanao na maambukizi ya virusi lazima ujitokeze ndani ya siku au majuma kadhaa au si zaidi ya mwezi 1, na hili siyo la kujadiliana, muda ambao virusi huhitaji kujirudufu na kusababisha ugonjwa ni lazima utokee ndani ya muda huo isipokuwa kama ugonjwa huo hautokani na virusi. Kwahiyo pengine kuna wanavirusi wa polepole (slow virologists) lakini siyo kirusi cha polepole.
6. VVU/HIV si kirusi kipya, hivyo hakiwezi kusababisha ugonjwa mpya:
Pengine watu wanadhani VVU/HIV kiligunduliwa miaka ya 1980 ulipoanza kutajwa Ukimwi.
Kesi za UKIMWI zilianza kutoka sifuri mwaka 1980 hadi kuripotiwa kesi nusu milioni katika Amerika ya Kaskazini peke yake mpaka kufika mwaka 1995. Kwa hiyo, wanasayansi wengine wanadai VVU/HIV lazima kitakuwa ni virusi kipya la sivyo tungekuwa na janga la ukimwi miaka ya karne iliyopita. Hata hivyo, madai haya yanaangushwa na kanuni za mwanasayansi Farr.
Kanuni ya Farr kwa magonjwa ya kuambukizana kwa njia ya virusi huenea kwa uwiano sawa katika idadi ya watu. Nchini Marekani maambukizi mapya ya VVU yameripotiwa kuwa zaidi au chini ya milioni 1 kila mwaka tangu vipimo vya kwanza mwaka 1984. Hivyo VVU/HIV hakiwezi kuwa kirusi kipya.
7. VVU/HIV kimefeli kanuni za Koch:
Kanuni  ya kimataifa inayotumiwa na wanasayansi kutambuwa iwapo ni kweli ugonjwa umesababishwa na maambukizi, ilitengenezwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita na mwanasayansi Robert Koch.
Kanuni hiyo ya Koch inasema:
Kiumbe (kirusi):
  • Lazima kipatikane katika matukio yote ya ugonjwa huo.
  • Lazima kijipoteze kutoka kwa mwenyeji wake na kujikuza binafsi
  • Lazima kisababishe ugonjwa ule ule sawa wakati kimedungwa kwa mwenyeji mpya mwenye afya.
  • Lazima kipatikane kinakua tena katika ugonjwa wa mwenyeji wake (host/cell).
  • Lazima mbegu za kirusi kupatikana katika matukio yote ya magonjwa. VVU/HIV KIMEFELI.
  • Asilimia 10 na 20 ya wagonjwa wa UKIMWI hawana VVU/HIV.
  • Ni kiasi kidogo tu cha VVU, kwa kawaida virusi mfu (dormant), ndiyo vinaweza kupatikana katika watu wenye UKIMWI.
  • Kadhalika ni lazima mbegu ya kirusi (germ) pekee itoke kwa mwenyeji na kukua na kuwa kirusi binafsi. Hili VVU/HIV KIMEFAULU – lakini katika baadhi tu ya watu sababu ya kiteknolojia.
  • Kiasi kikubwa cha tishu za seli zinahitajika ili kupata VVU. VVU/HIV kinahitaji mchakato wa kikemikali ikiwa ni pamoja na kuamka, kinyume chake, kiasi kikubwa cha virusi walioamshwa wanaweza kupatikana pamoja na virusi wengine.
  • VVU/HIV havisababishi UKIMWI/AIDS katika majaribio kwa wanyama kama sokwe.
  • Wahudumu wa afya ambao kwa bahati mbaya huambukizwa VVU wakati wakitimiza majukumu yao mara chache huugua Ukimwi isipokuwa kama ni watumiaji wa madawa ya kulevya au AZT.
  • Kadhalika ni lazima mbegu kupatikana ikiongezeka tena katika ugonjwa mpya unaoletwa na kirusi hicho hicho cha aina moja. VVU/HIV KIMEFELI Kanuni hii – kutokana na kuferi kanuni namba 3.
HIV/VVU imefeli kanuni hizi.
Wanasayansi wa VVU/UKIMWI wanadai kwamba Kanuni za Koch ni za zamani na zipo nje ya wakati (outdated) katika sayansi za kisasa. Lakini wao wamesimama na mitihani ya muda. Nadharia za magonjwa amabayo yamepuuza kanuni za Koch, zote zimefeli; nadharia ya kuambukiza ya kiseyeye (scurvy), pellagra, beriberi, SMON na utafiti juu ya virusi wa kansa, magonjwa haya yote yamefeli sababu za kupuuza kanuni za Koch. Na sasa VVU / UKIMWI?
8. UKIMWI umebakia ugonjwa wa makundi yale yale ya awali hatarishi kwa zaidi ya miongo 3:
Ikiwa ugonjwa hausambai, lazima uwe umesababishwa na kitu kingine kisicho cha kuambukiza. Kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC) kimethibitisha hilo katika taarifa yake mwaka (1997) kwamba UKIMWI hauenei sawa katika jamii nzima.
UKIMWI katika makundi hatarishi (Marekani, 1995/96):
  • Mashoga wanaume 54%
  • Watumiaji wa madawa ya kulevya (IV drug users) 32%
  • Hemofilia 1%
  • Waongezewa damu 1%
  • Mapenzi ya jinsia tofauti  9%
  • Watoto 1%
Jumla: 97%
IKiwa ni kweli UKIMWI unasababishwa na virusi vya Ukimwi, wagonjwa wa UKIMWI wasio katika makundi hatarishi walitakiwa wawe wanaongezeka zaidi ya wastani wa asilimia 10% kadiri ugonjwa unavyosambaa.
Kumbuka kwamba wakati jeshi la Marekani lilipokuwa likifanya vipimo kwa makuruta liligundua kuwa matokeo ya watu waliopima na kukutwa na VVU yalikuwa yamegawanyika hamsini kwa hamsini, asilimia (50%) wanaume na wanawake asilimia (50%). Hata hivyo, asilimia 85% ya wagonjwa wa UKIMWI nchini Marekani ni wanaume.
Kumbuka pia kwamba nchini Marekani wanaume hutumia zaidi ya asilimia 80 ya madawa yote makali ya kulevya. Kati ya wanawake wenye UKIMWI, asilimia 60% wanakiri kutumia madawa makali ya kulevya.
9. Uwiano wa watu wenye Ukimwi kimataifa unatofautiana sana.
Takwimu 3
Ugonjwa wa kuambukizana kadhalika utaleta uwiano wa idadi ya watu katika njia hiyo hiyo duniani kote. kuzuka kwa kipindupindu katika India na Honduras kutakuwa na kiasi hicho hicho. Lakini UKIMWI ni tofauti kabisa katika Marekani au katika nchi za viwanda za magharibi na nchi za Afrika
UKIMWI katika Afrika ulipaswa kuwa mara 14 juu kuliko katika Marekani. Badala yake, watu wenye VVU Marekani huanza kuugua UKIMWI kwa kasi zaidi mara10 hadi 20 kuliko katika Afrika. Hii ina maana kwamba, wakati muda wa kuishi kwa matumaini ukikadiriwa kuwa miaka 10 hadi 15 nchini Marekani, katika bara la Afrika ni angalau miaka 100-150!
10. UKIMWI hutokea bila ya maambukizi ya VVU na watu wengi wenye VVU kamwe hawaoneshi kuugua UKIMWI:
Ushahidi wa nadharia isemayo VVU =  UKIMWI imeegemea tu juu ya uhusiano (correlation). Sababu virusi/hiv hupatikana katika wagonjwa wengi wa UKIMWI, ikadhaniwa huenda hiv/vvu husababisha UKIMWI. Lakini mantiki ya dhana hii ina dosari kwa sababu uhusiano (correlation) hauwezi kuthibitisha Usababisho (Causation), ni kama kusema kila anayefaulu mitihani basi anajisomea sana!
Utokeaji wa kawaida wa VVU/HIV katika wagonjwa wa UKIMWI si ushuhuda tena kwamba VVU husababisha UKIMWI, ni sawa na kusema pia kunguru akisimama kwenye nyanya za umeme ni uthibitisho wa kukatika umeme!.
Hivyo, kama VVU na UKIMWI havihusiani, ni rahisi kupata watu wenye UKIMWI bila kuwa na VVU na watu wenye afya ambao wanaishi na VVU lakini kamwe hawauguwi UKIMWI. Na hicho ndicho kinachotokea.
Katika Afrika utafiti umeonyesha zaidi ya asilimia 65% ya wagonjwa wa UKIMWI hawana VVU. Katika Afrika vipimo chanya kwa HIV katika kinga ya mwili havina muhimu kwa ajili ya kuripoti wagonjwa wa UKIMWI; dalili za kuugua muda mrefu zinatosha.
Kesi  4,621 za UKIMWI bila VVU zimejitokeza katika Kituo cha kudhibiti magonjwa cha Marekani (CDC), ripoti ya hadi 1993. Na idadi inaweza kuwa kubwa zaidi lakini tafsiri rasmi ya UKIMWI imeundwa ili kuondoa kabisa UKIMWI bila ya V.V.U.
UKIMWI unatofautiana karibu na ugonjwa wowote ambao umewahi kutokea duniani kutokana na ukweli kuwa hauna dalili maalumu za ukweli za kudumu. UKIMWI ni neno mwamvuli kwa ajili ya magonjwa mengine zaidi ya 29 ya zamani na mmoja ambao siyo ugonjwa (wa chembechembe za seli T4 wa chini ya 200/ul ya damu) wakati mtu amekutwa na kinga dhidi ya VVU anapofanya vipimo vya ukimwi.
Namna tafsiri ya UKIMWI ya CDC inavyofanya kazi:
  • Kaposi sarkoma + HIV = UKIMWI
  • kaposi sarkoma – VVU = kaposi sarkoma
  • Pneumonia + HIV = UKIMWI
  • Pneumonia – VVU = Pneumonia
  • Dementia (matatizo ya akili) + HIV = UKIMWI
  • Dementia – VVU = Dementia
  • Chembechembe chini ya 200 za seli T4 + HIV = UKIMWI
  • Chembechembe chini ya 200 za seli T4 – VVU = hakuna ugonjwa
na kadhalika …
Hakuna ugonjwa ambao husababishwa na VVU/HIV pekee. HIV/VVU inasemwa husababisha magonjwa 29 ya zamani wakati inapokuwepo sasa inapojitokeza sambamba na magonjwa mengine. Wakati HIV/VVU hakijaanza kusemwa husababisha ukimwi, sababu za magonjwa hayo zaidi ya 29 zinajulikana, si VVU/HIV tena.
Tafsiri rasmi ya UKIMWI inajenga uhusiano wa asilimia 100% kati ya Ukimwi na virusi vya UKIMWI. Uhusiano (correlation) huo siyo lengo au jambo la kisayansi, bali ni usanii na ghiriba zilizojaa maslahi binafsi.

Je ni kweli UKIMWI ni ugonjwa wa kuambukizana?
Si kweli. Kwa miaka mingi watu wengi wamekuwa wakiamini kuwa ukimwi ni ugonjwa wa kuambukizana jambo ambalo si kweli. Tunachoamini ni kuwa, ni kweli kinga ya mwili huweza kupungua mwilini kiasi cha kusababisha magonjwa lakini si kweli kuwa V.V.U ndivyo vinavyohusika na kushuka kwa kinga hiyo.
Kama tulivyoona kwenye aya kadhaa hapo juu namna sayansi ya kweli inavyokataa V.V.U kuwa na uwezo wa kusababisha UKIMWI, kwahiyo kama V.V.U havina uwezo wa kusababisha ugonjwa wowote mwilini basi tunaweza kuhitimisha kuwa UKIMWI au Upungufu wa Kinga Mwilini si ugonjwa wa kuambukizana, kama kinga ya mwili wako itashuka basi itaanzia mwilini mwako na kuishia mwilini mwako humo humo, wewe huna uwezo wa kumwambukiza mwingine wala mwingine yeyote hana uwezo wa kukuambukiza wewe.

V.V.U au H.I.V ni nini?
HIV virus
“V.V.U ni kipande tu cha tishu pole mfu chenye ukubwa wa 1 ya 1000 ya ukubwa wa seli ya kawaida, siyo kama vilivyo virusi aina ya retrovirusi vingine vingi vilivyomo katika miili yetu …”
Watetezi wa dhana ya Virusi Vya Ukimwi kusababisha ukimwi wanadhani kwakuwa ukimwi umesambaa kwa kasi tangu mwaka 1981 basi V.V.U ndivyo vitakuwa vimesababisha hilo.
Lakini sayansi imefeli kuuliza swali moja rahisi; Je H.I.V imekuwepo katika mwili wa binadamu tangu mwaka gani?.
Tukitumia kile sayansi hukiita kanuni ya mwanasayansi Farrs (Farrs’ law) tunaweza kuona kuwa H.I.V imekuwepo kwa karne nyingi zilizopita.
Alichokisema mwanasayansi Farr kilikuwa kwamba wakati kirusi kinapojitokeza kuleta ugonjwa kwa binadamu huenea kwa kasi na kwa wote kama tulivyoona katika janga la virusi vya mafua ya ndege. Lakini kwa sababu tangu HIV ilipogundulika ni waMarekani milioni 1 tu ambao ndio wanasemwa kuwa na H.I.V kila mwaka kwa zaidi ya miaka 20 sasa na haionyeshi dalili ya kukuwa na kusambaa kwa wote, kirusi cha H.I.V hakiwezi kuwa ni kitu kigeni katika mwili wa binadamu.  H.I.V ni kitu cha zamani kuliko hata nchi unayoishi, kimekuwepo katika miili ya watu wengi na watoto wao kwa karne kadhaa kwa mjibu wa Farrs’ Law.

Hebu tuone sasa tangu mwanzo namna H.I.V ilivyogunduliwa na kusemwa husababisha ugonjwa usioponyeka wa UKIMWI.
Luc Montagnier daktari na mwanasayansi wa Ufaransa ndiye alikuwa wa kwanza kukibaini kirusi cha H.I.V mwaka 1982 na matokeo ya utafiti wake yakatumwa katika maabara huko Califonia Marekani kwa uchunguzi zaidi ambako daktari mwingine Robert Gallo mwenyewe binafsi akaeleza kuwa amekigunduwa kirusi hicho na akakipa jina HTLV 1, kwahiyo mwanasayansi huyo mfaransa akaamua kufunguwa mashtaka kwa upotoshaji wa Robert Gallo na wanasayansi hawa wawili wote ndio wanaosemwa kuwa waligunduwa aina hii ya kirusi cha kiretrovirusi kiitwacho H.I.V.
Muda mchache kabla ya janga la UKIMWI kutangazwa katikati ya miaka ya 1980 Dr.Robert Gallo  alikuwa ni mwanasayansi aliyekuwa akiendelea na utafiti juu ya ugonjwa wa kansa. Utafiti wake huo katika kansa ulifanana kwa karibu na utafiti wa UKIMWI. Dr Robert Gallo alikuwa akijaribu kuthibitisha kuwa kirusi kile kile kinachofanana na cha UKIMWI (HTLV 1) ndicho kilikuwa kikisababisha ugonjwa wa kansa. Utafiti wake huo upande wa kansa haukuzaa matunda na akashindwa kuthibitisha kwamba HTLV 1 ndicho kilikuwa kikisababisha kansa.
Dr.Robert Gallo akapata nafasi nyingine mwanzoni mwa 1980 tena kuthibitisha nadharia ya kirusi chake dhidi ya UKIMWI ambapo yeye na baadhi ya wanasayansi wengine jamaa zake walikuwa wakidai kwamba kirusi kiitwacho H.I.V kilikuwa kikizishambulia na kuziua T-Cells ambazo ni seli maalumu zinazounda mfumo wa kinga ya mwili wa binadamu. Na hata sasa Gallo ameendelea kudai H.I.V na virusi vingine vimekuwa vikiziuwa T-Cells na siyo H.I.V peke yake.

Kutoka katika kitabu kiitwacho Deadly Deception cha dr Robert E. Willner M.D., Ph.D:
H.I.V haisababishi UKIMWI…. Kitu ambacho kila mtu anakikosa ni kwamba hizo karatasi zote Gallo ameziandika kuhusu H.I.V na UKIMWI zimegundulika kuwa ni za uongo na nadharia kuhusu UKIMWI imeegemea katika hizo karatasi zake. — Dr. Peter Duesberg’.
Namna uongo ulivyoanza:
Mwaka 1980, Dr. Robert Gallo ambaye ni mwanaretrovirusi akiwa katika taasisi ya taifa ya kansa ya Marekani alidai alikuwa amegunduwa kirusi katika kundi la retrovirusi kiitwacho HTLV-I. Kirusi hiki cha retrovirusi kinatofautishwa na virusi vingine vya kawaida kutokana na sifa ya R.N.A yake kuweza kubadilika kuwa D.N.A kwa kimeng’enya (enzyme) kiitwacho kwa kiingerezareverse transcriptase’.
Kujizalisha, kuongezeka na kuishi kwake kwa retrovirusi kunategemea uhai wa seli ambayo hiki kirusi kimo ndani yake. Ikitokea seli inayokishikiria hiki kirusi inakufa basi hata kirusi nacho hufa pia. Dr. Gallo alikuwa akiujuwa ukweli huu ingawa kwa haraka na kwa makusudi aliamua kuudharau ukweli huu ili kutimiza malengo yake binafsi kwa kudai kwamba kirusi hicho kilikuwa ni kirusi cha maajabu sana kuwahi kutokea. Akaendelea kudai kuwa kirusi hicho cha ajabu kingeweza kudumu kimaajabuajabu kwa kuwaua mamilioni ya watu kitu ambacho hakijawahi kutokea.
Ikumbukwe kabla huyu jamaa alishindwa kuuthibitishia ulimwengu kuwa kirusi kile kile chake sawa cha HTLV 1 kilikuwa kikisababisha kansa ya damu (leukemia) nchini Japani. Sababu ya kuwa na nguvu za kimadaraka zile za kuwa mtu mkubwa na mwanasayansi serikalini, ndizo ziliruhusu kosa la lebo ya kirusi wa leukemia kukubaliwa kuwa ndicho kilikuwa kikisababisha leukemia hata baada ya jopo la wanasayansi kuikataa nadharia hiyo.
Mwaka 1980, ilikuwa ikipendekezwa kuwa upungufu wa kinga mwilini (acquired immune deficiency) ulikuwa ndiyo msingi wa dalili ya ugonjwa mpya ujulikanao kama UKIMWI ambao ulikuwa ukionekana kuwatokea zaidi wanaume mashoga na wale waliokuwa wakitumia madawa ya kulevya hasa yale ya kujidunga kwa sindano.
Dr. David Durack wa chuo kikuu cha DUKE, ambaye ni bingwa katika magonjwa ya kuambukiza na mfumo wa kinga ya mwili, anasema ingawa anakubaliana na uhusiano wa madawa ya kulevya kama ‘poppers’ na ‘amyl nitrites’ na maambukizi ya kujirudiarudia, alidharau hivyo vitu vinavyojulikana wazi kusababisha kushuka kwa kinga ya mwili na kutangaza kuwa hizi dalili mpya za kushuka kwa kinga ya mwili lazima ziwe zinaletwa na ‘jambo jipya’.
Kundi hili la wanasayansi hawa wamejifungia katika nadharia yao hiyo pasipo kuwa na ukweli wowote wa kisayansi kwamba ni kwa namna gani kirusi chao cha ukimwi (H.I.V) kinaweza kusababisha matendo machafu yote hayo mwilini.
Neno ‘inasadikika au kufikirika’ ndilo hutumika kila mara katika majibizano ya kawaida au katika majarida, magazeti na vitabu visivyo vya kisayansi. Katika majarida ya kisayansi au mafunzo ya kisayansi nadharia huwasilishwa kama ukweli uliothibitishwa na kwahiyo unakubalika hivyo na wanasayansi wengi ikijumuisha wanafizikia pia. Kumbe hicho kinachoitwa kirusi cha ukimwi (H.I.V) bado kinawasilishwa kama ni kirusi ‘kipya’ pamoja na ukweli usiopingika kuwa hakuna upya wowote hapo.
Kwa uongo mkubwa kirusi hicho kimekuwa kikielezwa kuwa ni kirusi kinachoshambulia na kudhuru kinga ya mwili wakati ukweli ni kuwa hilo haliwezekani kwakuwa kirusi hicho si kiumbe au kitu chenye uhai na wala hakina uwezo wa kushambulia kitu chochote mwilini. Virusi aina ya Retrovirusi humezwa na kujumlishwa katika maisha ya kila siku ya seli na kuwa na ukubwa wa 1/1000 ya ukubwa wa seli ya kawaida.
Mwaka 1983, Dr. Gallo alianzisha mpango mwingine wa kuwashawishi wanasayansi rafiki zake wengine bila kuwepo kwa ushahidi au uthibitisho wa kimajaribio ya kisayansi kwamba alikuwa amegunduwa kirusi kingine ambacho kilikuwa kikisababisha UKIMWI.
Kwenye mkutano mkubwa kabisa uliofanyika Washington, D.C. tarehe 23 aprili 1984, Dr. Gallo akatangaza kwamba amegunduwa kilichokuwa kinasababisha ugonjwa wa UKIMWI. Dr Gallo akanena juu ya ugunduzi wake wa kirusi kipya kundi la retrovirusi ambacho alikuwa amekipa jina HTLV-III, hivyo na kuhitimisha kwamba kirusi hicho kilikuwa ni miongoni mwa virusi kundi la retrovirusi alivyokuwa amevigunduwa kabla.
Madai yake haya yaliungwa mkono na Margaret Heckler, aliyekuwa Waziri wa afya na huduma za jamii ambaye alikuwa katika presha za kisiasa na kuja na jibu la ‘janga’ jipya. Waziri Heckler alitangaza; ‘Leo tunaongeza muujiza mwingine katika heshima ya muda mrefu katika dawa na sayansi ya kimarekani’, akaahidi pia kuwa kinga ya ugonjwa huo itakuwa imepatikana ndani ya miaka miwili inayokuja, bilashaka yeyote kama matokeo ya Dr. Gallo kulazimisha uongo kuwa ukweli.
Siku hiyo hiyo Dr. Gallo akajaza leseni ya kifaa cha kupimia UKIMWI ambacho kilikusudiwa kumtengenezea mamilioni ya pesa. Dr. Gallo mtu mwenye ujuzi mkubwa usiotiliwa shaka yeyote katika fani ya retrovirusi akachagua kuuweka ukweli pembeni na kuhalalisha baya kuwa zuri. Faida kwa Dr. Gallo ni pesa na nguvu lakini gharama kwa ubinadamu ni mateso na maelfu ya vifo visivyo vya lazima. Kinyume chake, wanawake malaya wa barabarani ni wakarimu zaidi – unakijuwa nini unachopewa na unayajuwa matokeo au gharama yake – na kwa hakika UKIMWI si mojawapo ya matokeo au gharama hizo.
Kwa haraka Margaret Heckler akatoa mkataba wenye faida kwa utengenezeaji wa dawa ya kupunguza makali ya UKIMWI iitwayo AZT kwa kampuni ya Burroughs-Wellcome Pharmaceutical Company kabla hata ya chapisho la kwanza la kisayansi kuhusu ugunduzi huo kutokea/kuchapwa kwenye majarida ya Marekani.
AZT ilikuwa ni dawa ikitafuta ugonjwa wa kutibu na ilikuwepo kwenye makabati ya taasisi ya taifa ya kansa ya Marekani tangu mwaka 1960. Dawa hiyo ilikuwa imetumika kwenye majaribio ya kutibu kansa na ikashindwa, kisha ilitolewa kwenye matumizi kufuatia kugundulika kuwa ina sumu nyingi sana kwa matumizi ya binadamu.
Fani ya Retrovirusi ilipata umhimu wakati huo kutokana na vita dhidi ya kansa kwa kampeni iliyoenda kwa jina la Nixon’s “War on Cancer” na imani kuwa retrovirusi ndiyo sababu au ndiyo chanzo cha kansa kwa binadamu. Imani hiyo ilionekana kuwa na mashiko kwa wakati huo kwa sababu retrovirusi vina tabia ya kuchochea seli kujizidisha au kuongezeka idadi – ambayo ni sifa mojawapo katika kukua kwa kansa. Hii ni tofauti ya moja kwa moja kwa uharibifu wa seli ambao kwa kawaida hutokea katika maambukizi yatokanayo na virusi.
Siyo kwamba ni hiyo vita pekee dhidi ya kansa ndiyo iliyofeli, AZT ilifeli pia, na wataalamu hao katika masuala ya retrovirusi wakaja mikono mitupu hata baada ya miaka 20 ya utafiti huo mkubwa na mzito. Cha kushangaza, Bila sababu yoyote ya mhimu (without a reason d’etre!) kundi zima la wanasayansi, kama ambavyo ungetegemea, mwaka 1986 katika mkutano mkuu wa kimataifa wa wataalamu wa retrovirusi  (The International Committee of Retrovirologists) wakaitaja H.I.V (V.V.U) kama ndiyo chanzo au ndicho kitu kinachosababisha ugonjwa wa UKIMWI (AIDS).
Kwa kuisadiki nadharia hiyo ya H.I.V kusababisha UKIMWI bila uwepo wa uthibitisho wa kisayansi wanamkutano huo wote wakawa ni sehemu ya hii njama chafu. Ni kama vile kila mmoja angeweza kutegemea nini kitatokea pale Mbweha waliochanganyikiwa kwa kukosa kitoweo kwenye mawindo yao wanapoachwa peke yao kulinda banda la kuku.
Ukiongeza sasa kwenye fujo za  Dr. Gallo kwa kudharau umhimu wa kuthibitisha kisayansi madai yake, ilikuja kugundulika kuwa  HTLV-III ilikuwa ni retrovirusi ambacho kilitumwa na daktari mwingine mfaransa Luc Montagnier wa Pasteur Institute ya Paris kwenda kwa Dr. Gallo zaidi ya mwaka mmoja kabla. Katika nyakati tofauti Montagnier alikuwa akituma sampuli za virusi alivyokuwa amevigunduwa katika damu za waathirika wa UKIMWI kwenda kwa Gallo kwa ajili ya utafiti zaidi.
Skendo hiyo ikavuma na ugomvi huo ulizuka juu ya mwenye kustahili kupewa cheo na hati miliki ya ugunduzi. Ilipelekea kuingilia kati kwa aliyekuwa waziri mkuu wa ufaransa wakati huo Jacques Chirac na rais wa Marekani Ronald Reagan ili kufikia makubaliano ambayo yalikuwa ni umiliki wa pamoja wa mapato yatokanayo na ugunduzi huo (hivi karibuni ufaransa ilitoa changamoto tena baada ya Gallo kukiri huenda alikuwa amefanya makosa), hii ni tabia ya kweli ya watu matapeli au watu wafanyao mambo maovu kwa maksudi ya wazi kugombana juu ya mali waliyoipata kilaghai.
Ni mhimu kuelewa hapa kuwa tangu mwanzo neno UKIMWI linawakilisha kifupi cha maneno ‘Upungufu wa Kinga Mwilini’ ambao ndio unaojadiliwa, kupelelezwa na kuhakikiwa katika makala hii. Hitimisho lisilopingika ambalo ongezeko kubwa la wanasayansi maarufu pia wamefikia ambalo nina uhakika ndilo utakalolifikia wewe pia, ni kwamba UKIMWI kamwe hauwezi kutafsiriwa na kukubalika kama ni ugonjwa au dalili za ugonjwa wa aina yeyote ile. UKIMWI ni kusanyiko na ongezeko la pamoja la idadi ya magonjwa na dalili zaidi ya 25 (kutegemea na chanzo) kwa ajili ya kujengea hoja ya kitapeli kwamba janga hilo lipo kweli.
Kitu kingine unachotakiwa kuelewa ni kuwa Gallo na kundi lake wamekuwa wakikimbia hatua moja ya msingi na mhimu kabisa katika sayansi, nayo ni kukataa kufanya majaribio yanayodhibitiwa ambayo matokeo yake ndiyo yatakuwa ni ukweli unaokubalika na wanasayansi wote kote duniani. Majaribio kama hayo yangeuanika ulaghai wao peupe. Badala yake wamekuwa ni watu wanaotegemea hofu, vitisho, vioja, tama za vyeo, uroho, husuda na tamaa ya umaarufu. Katika hali hii wamefanikiwa kulazimisha kutia ujinga jeshi kubwa la wafuasi katika kuamini kile ambacho miaka ya nyuma kingekuwa ni kitu cha kuchekwa tu au kuchukuliwa kama hadithi tu za kawaida.
Binadamu wote tumekuwa tukijijuwa zaidi ya nusu karne sasa kwamba wote tunaishi na kutembea na bakteria wengi na virusi katika miili yetu. Wote tunajuwa kuwa kwenye miili yetu tunaishi na vijidudu hatari muda wote wa maisha yetu vikisubiri tu usawa wa mwili kuwekwa katika hali ya kuvutia ugonjwa fulani. Magonjwa kama Streptococcus, kifua kikuu na vichomi, ni magonjwa yanayoweza kumpata yeyote muda wowote.
Vijidudu vya ugonjwa wa kifua kikuu kwa mfano vinaweza kuonekana karibu katika kila mapafu ya kila mtu. Lakini hata hivyo ni watu wachache kati yetu wanaugua ugonjwa wa kifua kikuu. Huu ni moja ya mifano mhimu kati ya magonjwa mengi yanayoitwa nyemelezi kwa watu wanaoishi na Virusi Vya Ukimwi magonjwa ambayo mengi kati yake kila mmoja amewahi kuugua mara moja au mbili katika kuishi kwake.
Hebu jiulize maswali yafuatayo kwa sasa:
Wakati mlipuko wa homa ya mafua makuu ya mwaka 1919 ulipochukua maisha ya mamilioni ya watu wa Marekani, kwanini hayakudhuru waMarekani wote kwa pamoja?
Wakati ugonjwa wa tauni ulipoangamiza theruthi moja ya idadi ya watu wa bara la Ulaya, kwanini theruthi zingine mbili ya watu hawakufa pia?
Kanuni kumi za ulaghai:
1. Ulinganifu ni uthibitisho wa chanzo na matokeo yake.
2. Ushahidi bila kithibitisho ni ukweli wa moja kwa moja.
3. Mfano mmoja tu unathibitisha kanuni.
4. Kisio (Dhanio) moja likisaidiwa na kisio jingine linatengeneza ukweli.
5. Kwa kukisema tu kitu kiko hivi, tayari hicho kitu lazima kiwe hivyo.
6. Usichanganye habari na ukweli.
7. Uthibitisho si kitu cha lazima na ni lazima uepukwe.
8. Ongopa, ongopa, ongopa na mwisho wataamini tu.
9. Wezesha ukimya, dharau na kanusha ukweli.
10. Weka imani (kitu kisichohakikiwa), ulaghai na upofu wa uwoga mahali pa mantiki.
Kurudiwarudiwa kwa matumizi ya hizi kanuni 10 za ulaghai na wala njama za H.I.V kuleta UKIMWI ndiko kulimpelekea T. C. Fry ambaye ni mwandishi wa kitabu kiitwacho The Great AIDS Hoax (Uongo Mkubwa kuhusu ukimwi), kuandika:  “Uwepo wa kile wanachokiita H.I.V katika ugonjwa wa UKIMWI si uthibitisho tena wa kinachosababisha UKIMWI zaidi ya uwepo wa inzi kwenye takataka kuwa si uthibitisho kwamba inzi ndizo zilizosababisha uwepo wa takataka hizo.”
Ingawa hilo lingewezekana kama utawachukulia hawa wahuni kina: Robert Gallo, Anthony Fauci, William Haseltine, Max Essex, James Curran, Flossie Wong-Staal, Dani Bolognesi, Margaret Fischl, Margaret Heckler na jamaa zao wengine kuwa ni ma-inzi na kwa hakika basi hata takataka (UKIMWI) zilitengenezwa na wao!.


No comments:

Post a Comment

advertise here