Wednesday, 24 June 2015

REKODI ZA KOCHA WA SIMBA ZAISHTUA TANZANIA

LAYIII
KOCHA mpya wa Simba, Dylan Kerr, anatarajiwa kutua nchini wikiendi hii akiwa anaonekana kuwa kocha mwenye rekodi kadhaa za ajabu kwenye soka. Kocha huyo anatua nchini kuchukua mikoba ya Goran Kopunovic, ambaye aliachana na timu hiyo ya Msimbazi baada ya kushindwana kwenye masuala ya kimaslahi.

REKODI 5 ZA KUSHTUA ZA KOCHA MPYA SIMBA


KOCHA mpya wa Simba, Dylan Kerr.
KOCHA mpya wa Simba, Dylan Kerr, anatarajiwa kutua nchini wikiendi hii akiwa anaonekana kuwa kocha mwenye rekodi kadhaa za ajabu kwenye soka. Kocha huyo anatua nchini kuchukua mikoba ya Goran Kopunovic, ambaye aliachana na timu hiyo ya Msimbazi baada ya kushindwana kwenye masuala ya kimaslahi.

Kerr, anakuja nchini akiwa ni kocha wa kwanza kwa miaka ya hivi karibuni kujiunga na Simba akitokea nchini Uingereza, lakini akiwa ana rekodi kwenye kila kitu, kucheza na kufundisha. Ajabu ni kwamba anakuja nchini akiwa ameshafundisha timu saba, lakini ni moja tu amekuwa kocha mkuu.
KUCHEZA: Kerr alikuwa beki wa kushoto wakati akicheza soka na alianzia kwenye timu maarufu ya Sheffi eld Wednesday, ambayo rekodi ya ajabu inaonyesha kuwa alijiunga nayo mwaka 1984 na kuondoka hapo mwaka 1988, lakini cha ajabu ni kwamba hakucheza mechi hata moja, hii ni rekodi ya kwanza.
REKODI YA PILI: Rekodi ya pili inaonyesha kuwa kwa kipindi cha miaka 19 ambacho kocha huyo alicheza soka, alifanikiwa kujiunga na timu 15, kubwa zikiwa ni Blackpool, Leeds na Reading, lakini inaonekana kuwa kwenye timu zote hizo, alifanikiwa kucheza michezo mingi akiwa na Reading ambayo ni 86 na kufunga mabao matano kwa kipindi cha miaka mitatu.
Timu iliyofuata hapa kwa mchezaji huyo kuitumikia michezo mingi ni Kilmarnock ambayo aliichezea michezo 61, timu hii inashiriki Ligi Kuu ya Scotland, ligi hii inashirikisha timu kama Rangers na Celtic. REKODI YA TATU: Kocha huyo anaonyesha kuwa hana uvumilivu kwani timu tatu kati ya hizo 16 alizitumikia kwa michezo mmoja mmoja, nazo ni Carlisle United, Kidderminster Harriers na East Stirlingshire.
Swali, nini kilikuwa kinamtimua? Na Simba atadumu? UKOCHA: Kwenye ukocha Kerr ana rekodi kama za kwenye kipindi chake cha kucheza soka, siyo mtulivu kwenye timu moja, lakini ameonekana kuwa ni mzuri sana wa kukaa nyuma ya watu, yaani msaidizi. REKODI YA NNE: Kerr alianza kufundisha soka mwaka 2009 ambapo alianzia kwenye timu inayojulikana kama Mpumalanga Black Aces ya Afrika Kusini akiwa kama kocha msaidizi.
Alidumu hapo kwa mwaka mmoja tu na kujiunga na Thanda Royal Zulu ya hapohapo Afrika Kusini akiwa pia msaidizi. Msimu uliofuata alikwenda Nathi Lions, pia kama msaidizi, mwaka mmoja mbele akaenda Khatoco Khánh pia kama msaidizi na mwaka 2012 akawa koch awa viungo wa timu ya taifa ya Viertnam, mwaka uliofuata ambao ni 2013 alijiunga na Hải Phòng kama msaidizi pia.
baada ya hapo akashushwa na kupelekwa timu ya vijana chini ya miaka 21, baada ya kocha mkuu kuondoka akawa kocha mkuu hadi mwaka jana, kumbuka kipindi hicho kilikuwa cha mwaka mmoja tu lakini
akatumika kwenye nafasi tatu.
Hali inaonyesha kuwa amekuwa kocha mkuu kwa mwaka mmoja tu na baada ya hapo hajawahi kuwa kocha mkuu tena zaidi ya sasa kuja kujiunga na Simba. REKODI YA TANO: Akiwa mchezaji kocha huyo alifanikiwa kutwaa makombe mawili, moja akiwa Reading na lingine alitwaa akiwa na Kilmarnock. Upande wa kocha, amefanikiwa kutwaa kombe moja la Ligi Kuu ya Viertnam mwaka jana akiwa na Hải Phòng.

No comments:

Post a Comment

advertise here