Wednesday, 24 June 2015

ATLETICO MADRID WASAJILI MSHAMBULIAJI MPYA

LAYIII
Siku chache baada ya kushuhudia mshambuliaji wake raia wa Croatia Mario Mandzukic akihamia nchini Italia kwenye klabu ya Juventus , mabingwa wa Hispania kwa msimu wa mwaka 2013/2014 Atletico Madrid hii leo wamethibitisha kumsajili mshambuliaji raia wa Colombia Jackson Martinez toka Fc Porto ya nchini Ureno 

Atletico Madrid wasajili mshambuliaji mpya .

Jackson-Martinez

Siku chache baada ya kushuhudia mshambuliaji wake raia wa Croatia Mario Mandzukic akihamia nchini Italia kwenye klabu ya Juventus , mabingwa wa Hispania kwa msimu wa mwaka 2013/2014
Atletico Madrid hii leo wamethibitisha kumsajili mshambuliaji raia wa Colombia Jackson Martinez toka Fc Porto ya nchini Ureno .
Martinez amekuwa akitajwa kwenye vichwa vya habari za michezo akihusishwa na kujiunga na klabu kadhaa kubwa barani ulaya ikiwemo Arsenal na Ac Milan na kuna wakati iliaminika kuwa yuko karibu kujiunga na Ac Milan ambayo imekuwa ikisaka wachezaji wa kurudisha hadhi yake iliyopotea .
Mshambuliaji huyu mwenye umri wa miaka 28 amekuwa na rekodi nzuri ya ufungaji kwenye ligi ya Ureno tangu alipojiunga na Fc Porto ambapo kwa misimu minne amefunga mabao 67 kwenye ligi huku msimu uliopita akifunga mabao 7 kwenye mechi 8 za michuano ya ligi ya mabingwa barani ulaya ambapo Porto ilifika hatua ya robo fainali .
Martinez anakwenda Atletico Madrid kuziba pengo la mshambuliaji Mario Mandzukic ambaye amedumu kwenye klabu hiyo ya katikati ya mji mkuu wa Hispania kwa muda wa msimu mmoja tu tangu aliposajiliwa toka Bayern Munich ya Ujerumani .
Zaidi ya Hapo Martinez anafuata nyayo za mshambuliaji mwingine wa Colombia Radamel Falcao ambaye aliwahi kupita Atletico Madrid kabla ya kujiunga na As Monaco na kisha Manchester United na hivi karibuni atajiunga na Chelsea ya England .

 

No comments:

Post a Comment

advertise here