LAYIII
Yule mwanaume aliyezaa na Staa wa Bongo Movies na Fleva,Shilole,aitwaye
Elias Makala ameibuka na kuzungumza na U heard na Soudy Brown kuwa
hakuwahi kumbaka msaniii huyo kama ambayo anazungumza kwenye vyombo vya
habari.
Mwanaume aliyezaa na Shilole Atoboa Haya Kuhusu Yeye na Shilole
ule mwanaume aliyezaa na Staa wa Bongo Movies na
Fleva,Shilole,aitwaye Elias Makala ameibuka na kuzungumza na U heard na
Soudy Brown kuwa hakuwahi kumbaka msaniii huyo kama ambayo anazungumza
kwenye vyombo vya habari.
‘’Mimi namshangaa sana Shilole anavyosema kuwa nilimbaka,sijawahi
kumbaka nilikuwa naishi naye kama mume na mke kwa zaidi ya miaka saba,
na nilimuuliza kwanini anasema uongo kuwa nilimbaka alinijibu kuwa
habari hiyo inamsaidia kumpaisha (kick) kwenye muziki wake,’’alisema
Makala.
Hata hivyo alipoulizwa kama anasikia wivu anasikia na kumuona Shilole
akila raha na mpenzi wake mpya msanii Nuh Mziwanda alisema kuwa haoni
wivu kwa kuwa Nuh anakula makombo yake kwani yeye ndiye aliyeanza kuwa
na msanii huyo.
‘’Sioni wivu kabisa miye ndiyo niliyeanza huyo Nuh anakula makombo
yangu,hata hivyo mimi nina mke na familia yangu huku Igunga,’aliongeza
Makala.
Msanii Shilole alipoulizwa alisema kuwa hawezi kumzungumzia mwanaume
huyo ambaye hajui kama mtoto wake anaishi vipi,anasoma wapi, na anakula
nini.
‘’Huwa sipendi kabisa kumzungumzia mwanaume huyo ambaye hajui mtoto
wake anaishi vipi,anasoma wapi na anakula nini,’’alijibu Shilole.