KATIKA MASHINDANO YA CCOPA AMERICA CHILE YACHUKUA USHINDI
LAYIII
Chile imewashinda Argentina kupitia kwa mikwaju ya penalti na kushinda
kombe kubwa zaidi kati ya nchi za Marekani ya kusini la Copa Amerika.
Hili ndilo kombe la kwanza la kimataifa kuwahi kushindwa na Chile.
Ni miaka 22 tangu Argentina washinde kombe lolote kubwa kwenye mashindano ya kandanda ya kimataifa.
Mchezaji wa Arsenal Alexis Sanchez alifunga bao la ushindi baada ya
mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain kupiga nje huku mkwaju wa Ever
Banega ukinyakwa na kipa Claudio Bravo. Awali Higuain alikuwa amekosa bao la wazi aliposalia na kipa baada ya dakika 90 za mchezo.
No comments:
Post a Comment