LIKE PAGE YETU HAPA
Dar es Salaam. Uhaba wa sukari umeendelea kushika kasi nchini
baada ya wafanyabiashara wa maduka ya jumla kuanza kuuza kwa rejareja,
huku ile nyeupe kutoka India ikipatikana kwa urahisi katika baadhi ya
maduka.
Utafiti uliofanywa na waandishi wa gazeti hili jijini Dar es Salaam, Kahama mkoani Shinyanga na wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro, bei ya sukari imeendelea kuwa juu huku upatikanaji wake nao ukiwa wa shida.
Baadhi ya wafanyabiashara walihojiwa walibainisha kuwa bei ya sukari kwa kilo, inaanzia kwa Sh2,500 hadi 3,900, na bei hiyo imetofautiana kulingana na aina ya sukari. Sukari nyeupe inauzwa kwa Sh120,000 kwa mfuko wa kilo 50 na Sh2,500 kwa kilo kwa bei ya rejareja.