Friday 27 May 2016

WANASAYANSI WA CHINA WANATUMIA NGURUWE KUTIBU UPOFU

LIKE PAGE YETU HAPA 
https://youtu.be/v3D2frsodIk
Wanasayansi wa Uchina wamefaulu katika tiba yao mpya ya majaribio ya kutibu upofu.
Walitumia nguruwe katika majaribio hayo ya tiba ya kuondoa upofu, ambapo walitumia konea kutoka kwa wanyama hao.
Sasa wamesema wana imani kwamba hilo litafaa sana kutokana na uhaba wa konea za binadamu.
Inakisiwa kuwa Wachina wapatao 5 milioni wanakabiliwa na matatizo ya konea, sehemu ya mbele ya jicho iliyo ngumu na inayowezesha miali ya mwanga kupenya.
Lakini ni konea 5,000 pekee ambazo hupatikana kila mwaka.

Matatizo ya konea husababisha watu wengi kuwa kipofu.Nguruwe
Njia hiyo mpya ya kutibu upofu imeanza kutumiwa baada ya kuidhinishwa na serikali mwaka jana.
Konea kutoka kwa nguruwe hutibiwa na kutolewa bakteria na virusi, pamoja na kutolewa DNA ya nguruwe, kabla ya kupandikizwa katika jicho la mwanadamu.
Wakosoaji wa mpango huo wanasema Uchina inaenda kwa kasi sana, bila kuangazia madhara ya mpango huo kwa kipindi kirefu.


No comments:

Post a Comment

advertise here