Bonyeza picha hapo chini kushuhudia video kali ya chura hapo
STAA wa Muziki wa Bongo Fleva, Snura Mushi ‘Chura’ juzikati akiwa kwenye shoo iliyofanyika Masasi, Mtwara alijikuta katika wakati mgumu baada ya kutaka kupigwa na mashabiki kisa kikiwa eti ni kutokuimba Wimbo wa Chura ambao umefungiwa.

Kwa mujibu wa chanzo, tukio hilo lilijiri mida ya usiku katika ukumbi mmoja maarufu uliopo Masasi ambapo
Snura alikuwa akifanya shoo hapo na alipotaka kumaliza, mashabiki
walimtaka amalize na Wimbo wa Chura ndipo kizaazaa kilipoanzia na kutaka
kumpiga
.
Baada ya kunyaka ubuyu huo, Over Ze
Weekend lilimnyanyulia simu Snura ambaye simu yake iliita bila
kupokelewa lakini alipopigiwa meneja wake, Hemed Kavu ‘HK’ alipokea na
kukiri kutokea kwa tukio hilo.
“Siyo tukio moja tu, tulishaenda shoo
zaidi ya mbili tunakutana na dhahama hizi. Tatizo lililopo, Snura hawezi
kupafomu wimbo ule kwa kuwa ulizuiliwa kutokana na video yake. Ni muda
umepita
video mpya imetengenezwa na kupelekwa bodi ya filamu kukaguliwa
lakini hawajatoa jibu lolote zaidi ya kuzungushwa tu, mara TCRA mara
Basata,” alisema HK.
PLAY VIDEO YA CHURA HAPA HAPA
No comments:
Post a Comment