Uchunguzi wa kidaktari kutoka jimbo
la Minnesota nchini Marekani umebaini kuwa mwanamuziki Prince alikufa
kutokana na kuzidisha kiwango cha dawa.
Kwa mujibu wa madaktari
waliofanya uchunguzi huo wa kifo cha mwanamuziki Prince, wanasema
alizidisha kiwango cha dawa za kutuliza maumivu zijulikanazokama
Fentanyl .Dawa hizo zinadaiwa kuwa na nguvu mara hamsini zaidi ya dawa za kulevya za Heroin.
Hata hivyo dawa hizo hutumika wakati wa upasuaji na hasa wagonjwa ambao miili yao ni sugu kwa
dawa nyingine za kutuliza maumivu.
Prince alikutwa amefariki dunia mwezi april mwaka huu, ndani ya lift katika makazi yake huko karibu na mji wa Minneapolis .
Siku moja kabla ya kifo chake inadaiwa kuwa alikuwa akihitaji msaada kutokakwa daktari maalumu kutokana na maumivu aliyokuwa akiyasikia.
Polisi wanaendelea na uchunguzi zaidi kutokana na kifo cha Prince
No comments:
Post a Comment