LAYIII
Zimebaki siku kadhaa nchi ya Kenya kutembelewa na Rais wa taifa lenye nguvu kubwa Duniani, nchi ya Marekani Barack Obama.
Tayari taarifa za kuwepo kwa ulinzi
mkubwa na wa hali ya juu zimesambaa kwamba mpaka sasa maafisa usalama
wapatao 800 watakuwepo wakitokea nchini Marekani.
Inasemekana kwamba serikali ya Kenya imesha andaa polisi zaidi ya 2000 kwa ajili ya ulinzi kwenye ziara hiyo ya Rais Obama.
Nchi ya Kenya imekuwa na matukio ya kigaidi mara kwa mara hivyo ulinzi kama huo ni muhimu hususani kwa ugeni mkubwa kama huo.
Ikumbukwe ya kwamba bajeti ya nchi hiyo kwa mwaka huu kiasi kikubwa
kimeelekezwa kwenye sekta ya ulinzi na hii ni kutokana na matukio
yanayohusishwa na ugaidi ya mara kwa mara yaliyotokea nchini Kenya kwa
siku za hivi karibuni.
No comments:
Post a Comment