Friday, 13 November 2015

WANAWAKE WAZURI HAWAOLEWI KUNAUKWELI WOWOTE? UNGANA NAMI HAPA

LAYIII
Si mara zote uhusiano wa ndoa ni matokeo ya upendo kama inavyotarajiwa. Yapo mahusiano mengi tu ya ndoa ambayo kimsingi ni arrangements za watu kujipatia mahitaji mengine kabisa yasiyohusiana na mapenzi. Ndoa zimeanza kuwa 'fursa' za kujinufaisha kibinafsi na zinameanza kupoteza dhana halisi ya mahusiano. Ndoa zimeanza kuchukuliwa kirahisi kama ubunge na udiwani unaopatikana hata kama huwapendi wapiga kura.

BONYEZA PICHA HII KUONA WANAFUNZI WALIOKAMATWA WAKIFANYA MAPENZI DARASANI  18+ NA ADHABU WALIO CHUKULIWA KAMA FUNDISHO KWA WENGINE


Leo nataka tujadiliane kuhusu mada ambayo siyo ngeni lakini imekuwa ikisababisha mivutano na migongano mingi ya kimawazo mara kwa mara kila inapojadiliwa, hasa na wanaume au wanawake wenyewe.
Hivi umeshawahi kujiuliza mwanamke mzuri anapaswa kuwa na vigezo vipi? Tukizungumzia mwanamke mzuri, kichwani mwako unajenga taswira gani?
WENGI WANADANGANYIKA NA SIFA ZA NJE
Ukipata nafasi ya kuzungumza na wanaume na kuwauliza wanawake wazuri wakoje, majibu utakayoyapata yatakushangaza. Wengi watazungumzia wanawake wenye sura nzuri, weupe sana, weusi wenye mvuto, wenye maumbo yanayokaribia kufanana na namba nane au ‘waliojazia’.
Si kila anayeolewa ni ‘wife material’

Kwanza haiwezekani kila mwanamke awe wife material. Tofauti ya malezi, imani, mitazamo na mambo mengine kibao, kama usawa wa kijinsia unaopiganiwa siku hizi, vyote hivyo vimewafanya wanawake wasikidhi vigezo vya kuoleka achilia mbali kuolewa kwa sababu ya kuwa na sifa za kuolewa. 

Na kama tulivyoona katika aya zilizopita, yapo mazingira ya kutosha kuwafanya wanawake kuolewa kwa sababu nyinginezo nje ya ‘kuwa na sifa za kuolewa’. Pengine wanacho kile kinachotafutwa na baadhi ya wanaume wanaojali ‘mengineyo’ zaidi ya upendo. Hivyo wanaolewa kama bidhaa, vitu, viwanda, wafanya kazi na kadhalika. 

Ndio maana unaweza kushangaa wanawake wajeuri, wazinzi, wababe, wasiopenda kwa dhati, bado wanaweza kuolewa kwa sherehe kubwa tu. Kwa nini? Ni kwa sababu wanaume wanaowaoa wanaotafuta bidhaa. Kwa wanaume wa jinsi hii wala usishangae wanawake wenye nidhamu, unyenyekevu na maadili wakaonekana si lolote.


No comments:

Post a Comment

advertise here