LAYIII

Mkurugenzi wa Yamoto Band na Wanaume Family, Said Fella aka Mkubwa Fella
alionesha mapema kabisa leo July 15 amechukua fomu ya kugombea udiwani
wa katika mtaa wa Kilungule, Wilaya ya Temeke Dar es Salaam.
Said Fella ameamua
kuchukua fomu hiyo na kugombea nafasi hiyo ili aweze kutatua kero za
wakazi wa kata ya Kilungule na kuleta maendeleo katika Kata hiyo.
“Nimeamua
kuchukua nafasi hii ili kutatua kero za kata yangu, hapa kuna shida ya
maji na barara naamini nikiwa Diwana nitaweza kuonana na wakubwa wa nchi
uso kwa macho na kuweza kuelezea shida za kata yangu, chamsingi ni
kuleta maendeleo“ – Said Fella.
Said Fella akisaini kitabu cha wageni mara alipofika katika ofisi za Kata ya Kilungule Wilaya ya Temeke
Katibu wa Siasa na Uenezi Kata ya Kilungule, Juma Ally Kilindo akimkabidhi fomu ya kuomba kugombea udiwani Said Fella
No comments:
Post a Comment