Thursday 16 July 2015

Hii ni good news kwa mashabiki wa Azam FC

LAYIII
Jean Baptiste Mugiraneza ni kiungo wa kimataifa wa Rwanda aliyesajiliwa na klabu ya Azam FC msimu huu akitokea klabu ya APR ya Rwanda kwa mkataba wa miaka miwili. Awali taarifa zilitoka kuwa kiungo huyo atarejea Rwanda kujumuika na kuitumikia timu yake ya APR katika mashindano ya kombe la Kagame yatakayoanza july 18 jumamosi hii.
Ila mambo yamekuwa tofauti baada ya klabu ya APR kumruhusu aichezee Azam FC katika mashindano ya kombe la Kagame. APR ambayo ipo kundi B n
a klabu za Al-Shandy ya Sudan, LLB AFC ya Burundi, Heegan Fc ya Somalia tayari imewasili jana Dar Es Salaam kwa mashindano hayo. Wakati kundi A kuna timu za Yanga Sc, Gor Mahia ya Kenya, Telekom ya Djibout, KMKM ya Zanzibar na Khatourm-N ya Sudan . Azam Fc wamepangwa kundi C lenye klabu za Malakia ya Sudani Kusini, Adama City ya Ethiopia na KCCA ya Uganda.
Hata hivyo Migi ambaye tayari uwezo wake umeonekana kwa kocha Stewart Hall na kujiunga na Azam FC anakuwa mchezaji wa kwanza wa kigeni kusajiliwa na Azam Fc msimu huu. Azam wamesajili jumla ya wachezji watatu tu hadi sasa ambao ni Ramadhani Singano kutoka SimbaAme Ali “Zungu” kutoka Mtibwa na Migi na kubakiwa na nafasi mmoja pekee ya kusajili mchezaji wa kigeni inayowaniwa na golikipa Nelson Lukong Bongaman kutoka Cameroon, Allan Watende Wanga kutoka Kenya, Ryan Burge kutoka Uingereza na Vincent Atchouailou de Paul Angban kutoka Ivory Coast.
Hata hivyo Wanga na Lukong wamegomea kufanya majaribioa licha ya kocha Stewart Hall kugoma kumsajili mchezaji ambaye hajamuona akicheza, hivyo Wanga na Lukong wanakuwa bado hawajui hatima yao kama watasajiliwa bila kufanya majaribio au ndio mpango wao wa kujiunga na Azam Fc umeishia hapo.
CHANZO CHA HII STORY>>>>BIN ZUBEIRY SPORTS- ONLINE

No comments:

Post a Comment

advertise here