Thursday, 16 July 2015

MAISHA YA WANAFUNZI HATARINI HUKO BUKOBA................KASHAI, BUKOBA

LAYIII
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kashai, mjini Bukoba,  wakiendelea kuchota maji kwenye mto Kashai karibu na mtaro wa maji machafu.

Shughuli ya kuchota maji ikiendelea kama kawaida siku zote.
Pamoja na hatari ya maji hayo wanafunzi bado wanaendelea kuyachota maji hayo ambayo huenda kuyatumia katika shughuli mbalimbali shuleni hapo.
Hili ni dampo lililo karibu na mto huo ambalo limejaa takataka za kila aina.
Dampo linalopitisha maji machafu na takataka lililopo eneo la Kashai Sokoni, jirani na kabisa na shule ya Msingi Kashai katika Manispaa ya Mji wa Bukoba limekuwa kero kubwa kwa wakazi wa eneo hilo na tishio kwa afya za wanafunzi wa shule hiyo.
Hali hiyo imekuwa ikisababisha harufu kali zinazotokana na maji machafu na takataka za mabaki ya chakula na vitu vingine vilivyooza kutupwa ndani ya dampo hilo na kupelekwa mpaka kwenye mto.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Kashai wamekuwa wakichota maji kwenye mtaro huo kwa matumizi mbalimbali ya shuleni kwao ikiwemo kumwagilia miti na maua, kusafishia vyumba vya madarasa na kazi nyinginezo, jambo ambalo linahatarisha afya ya watoto hao kutokana na kutumia maji ya mto yanayotoka kwenye dampo hilo.

No comments:

Post a Comment

advertise here