MAPYA YAIBUKA LOWASA KILELENI TENA KISA NI KINGUNGE
LAYIII
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru amesema CCM
inamuhitaji Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenye mchakato wa
Uchaguzi Mkuu na kukitaka chama hicho kujadili jambo hilo ili kuondoa
tofauti zilizojitokeza kabla ya kupiga kura za kumchagua Rais na
wabunge.
#newsflash CCM inamhitaji Lowassa ili Ishinde uchaguzi- Kingunge
Mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru amesema CCM
inamuhitaji Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa kwenye mchakato wa
Uchaguzi Mkuu na kukitaka chama hicho kujadili jambo hilo ili kuondoa
tofauti zilizojitokeza kabla ya kupiga kura za kumchagua Rais na
wabunge.
Katibu huyo wa zamani wa halmashauri Kuu ya CCM amesema Kamati ya
Maadili na Usalama iliteka majukumu ya Kamati Kuu baada ya kuamua
kuchuja majina ya makada waliojitokeza kuwania urais kwa tiketi ya chama
hadi kufikia watano, akisema jitihada hizo zilizofanywa kuvunja kanuni
zililenga kumuengua Lowassa kuwania kuingia Ikulu.
Akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake jijini Dar es
Salaam jana, Kingunge, ambaye alijitokeza waziwazi kumpigia debe
Lowassa, alisema kitendo cha kumuengua Lowassa kwa kuvunja kanuni
kimeacha kasoro kubwa ndani ya chama hicho tawala kwa sababu taratibu
zilikiukwa ili kupata viongozi.
Alisema kosa hilo si la Dk John Magufuli aliyepitishwa kuwa mgombea
urais wa CCM, na wala si la Lowassa, bali ni la waliopendekeza majina ya
walioingia tano bora.
Jina la Lowassa, ambaye alijidhihirisha kukubalika ndani na nje ya
CCM kutokana na harakati zake za kusaka wadhamini kujaa watu,
halikupelekwa kwenye Kamati Kuu, kwa mujibu wa Kingunge na hivyo
kutojadiliwa na chombo hicho ambacho kilimpitisha Dk Magufuli, Dk Asha
Rose Migiro, January Makamba, Bernard Membe na Balozi Amina Salum Ali.
“Jitihada zote ambazo zimefanywa za kuvunja taratibu zilikuwa
zinaelekezwa kwenye kumzuia Lowassa asipate haki. Badala ya yote nani
kashinda? Kashinda Lowassa kwa sababu imeonekana wazi kuwa yeye ndio
kipenzi cha Watanzania na hakuna kitu kikubwa kama kupendwa na watu,”
alisema.
“Kuanzia sasa wana-CCM tutafute namna ya kushikamana vizuri,
tuimarishe umoja wetu maana ndio nguvu yetu na katika hili ndugu Lowassa
ana nafasi muhimu na ya kimkakati ana mamilioni ya Watanzania wana
imani naye. “Mpaka sasa tunaulizwa maswali kutoka pande zote za nchi,
hatuna majibu. Tukitaka kufanikiwa kama chama tuunde mazingira
yatakayotuwezesha kutumia nguvu tulizonazo twende katika uchaguzi na
tushinde kwa kishindo. Lakini lazima yaliyotokea yazungumzwe ndani ya
chama maana tunahitaji ushirikiano wa Lowassa.”
Akielezea utaratibu wa uteuzi wa wagombea, Kingunge alisema
Halmashauri Kuu ya CCM ndiyo inachagua Kamati Kuu ya chama inayoitwa
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa na ndiyo ambayo inaunda chombo
cha Halamshauri Kuu ya Taifa kinachoitwa Kamati Kuu.
Alisema pia Halmashauri Kuu inaunda Sekretarieti ya Halmashauri Kuu
ya Taifa, kwamba ndani ya CCM vipo vitengo ambavyo vinahudumia vikao,
kikiwamo cha Kamati ya Maadili.
Alisema kwa utaratibu wa kikatiba, kazi ya sekretarieti ni kuhudumia
Kamati Kuu na Halmashauri Kuu ya Taifa, katika kupitisha wagombea urais,
Sekretarieti hukusanya majina ya walioomba kugombea na kuwasilisha
taarifa yake kwenye Kamati Kuu.
“Sekretarieti si kikao cha maamuzi, wala si kikao rasmi cha
mapendekezo. Mchakato hasa unatakiwa uanzie kwenye Kamati Kuu na ndiyo
utaratibu uliotumika mwaka 1995. Wagombea wote wanatakiwa kupita Kamati
Kuu na kila mmoja kujieleza sababu za kutaka kugombea urais,” alisema.
Katika kuteua mgombea urais wa CCM, vikao vya Kamati ya Maadili na
Usalama, Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu vilipishana kwa
muda mfupi kutoka kikao kimoja hadi kingine na kufanya suala hilo
liamuliwe katika muda wa siku mbili.
#magazetini #mwananch
No comments:
Post a Comment