Friday, 17 July 2015

KUTANA NA UCHAMBUZI WA MAGAZETI YA LEO TAREHE 17/07/2015 HAPA MTU WANGU

LAYIII
SAUTI ZOTE NIMEKUWEKEA HAPA MTUWANGU WA UKWELI
999
Inawezekana ulikuwa mbali na redio yako na uchambuzi wa magazeti kupitia @Clouds.Fm umekupita, nimefanya juhudi za kukurekodia zile zote kubwa zilizosikika leo kwenye @Power breakfast….
Mgombea Urais kupitia CCM Dk. John Magufuli jana apokelewa kwa kishindo Zanzibar na fukutu la kuchukua fomu za Ubunge zimeanza rasmi jana.
Wadau wa aliekuwa Waziri Mkuu wa zamani “Friends of Lowassa” watangaza kuhama CCM na kuhamia CHADEMA baada ya kutoridhishwa na mchakato wa kumtafuta mgombea Urais kupitia CCM.
Chama cha mabasi TABOA kimesema kunaweza kutokea mgomo wa mabasi kwenda mkoani kama Serikali haitopunguza tozo ya ushuru wa mabasi.
Kuna utafiti umefanyika na umebaini kuwa 65% ya wazazi wengi Dar es salaam wangependelea kiingerza kifundishwe kuanzia shule ya msingi.
Jeshi la polisi nchini linaendelea na upepelezi juu ya tukio la Sitakishari huku ulinzi wa vituo vyote vya polisi jijini umeimarishwa.
Sauti ya stori zote hizi nimekurekodia na kukuwekea hapa chini.


No comments:

Post a Comment

advertise here