Friday, 17 July 2015

WAJUE ALIENS HAPA MTU WANGU

LAYIII

Makala na Sifael Paul
MPENZI msomaji ungana nami katika simulizi hii mpya ya kweli inayohusu viumbe wa ajabu waishio angani. Kama ni msomaji wa vitabu vitakatifu, Mungu aliumba vitu vinavyoonekana na visivyoonekana. Inahisiwa kuwa visivyoonekana ni vingi kuliko vinavyoonekana.
Viumbe hao wa ajabu waishio angani wanaitwa Aliens. Wana muonekano kama binadamu isipokuwa hawafanani moja kwa moja na binadamu. Viumbe hao waliogundulika karne kadhaa zilizizopita
wameshatengenezewa filamu nyingi na wasanii mbalimbali duniani (tutazichambua huko mbele).
Aliens wapo wa rangi tofauti kama kijani, weupe, weusi, njano, zambarau na kila aina ya rangi.
Inaaminika kuwa Aliens wanaoishi angani wana akili nyingi kuliko binadamu. Wana mfumo wa kompyuta uitwao Alien Software na wapo juu kiteknolojia kuliko binadamu, tatizo tu hawavai nguo!
Tofauti na binadamu ambaye anafanya kazi kwa hatua moja kwenda nyingine, Aliens wao hufanya mambo kinyume kabisa. Kwa mfano wakitaka kusema ‘naomba maji’ husema ‘maji naomba’ yaani cha nyuma kinakwenda mbele na cha mbele kinarudi nyuma. Kama tunavyowashangaa, nao pia wanatushangaa na kutuona viumbe wa ajabu.
Wachambuzi wa mambo ya anga walishaandika ripoti nyingi kuhusu viumbe hao ambao huja duniani na kurudi angani.
Swali ni je, viumbe hao wanaishi katika sayari gani? Wataalam hao wanalijibu swali hilo kwa kusema haijulikani moja kwa moja wanaishi sayari gani lakini kwa uhakika siyo kwenye mwezi (kumbuka mwezi siyo sayari).
Inawezekana bado hujaelewa simulizi hii. Bermuda Triangle ni eneo la pembetatu la bahari lililopo kati ya nchi tatu katika Bahari ya Atlantiki. Miaka kadhaa huko nyuma viumbe hao waliwahi kutua eneo hilo na kuweka historia (nitaisimulia huko mbele).
Pia waliwahi kuonekana Kisiwa cha Bermuda pwani ya Mashariki mwa Marekani, Kisiwa cha Puerto Rico kilichopo Kaskazini mwa Carrebian na Fort Lauderdale huko Florida, Marekani.
Umewahi kusikia vitu mbalimbali duniani vikisemekana vimepotea katika mazingira ya kutatanisha? Aliens wanahusishwa na upoteaji wa meli baharini hasa za mizigo huku watu wakiamini huwa zinazama lakini uchunguzi ukifanyika meli hizo huwa hazionekani hata ndani ya maji baharini.
Aliens wanatajwa kuhusika na upotevu wa watu duniani ikiaminika kuwa labda watu hao walikufa lakini ukweli ni kwamba huchukuliwa na viumbe hao.
Ndege za kijeshi zimeripotiwa mara nyingi kupotea au kutokuonekana milele katika eneo la Bermuda Triangle ikieleza kuwa Aliens ndiyo wahusika wa upotevu huo.
Ujio wa Aliens katika eneo la Bermuda Triangle ulisababisha kisiwa hicho kupata umaarufu duniani na kupewa jina la Devil’s Sea (Bahari ya Shetani) ambapo binadamu wamekuwa wakiamini au kujenga imani potofu kuwa shetani amekuwa na makazi katika eneo hilo na kuwapoteza wasafiri wa majini. Wengine huhisi ni ushirikina.
Wapo binadamu wanaoamini kuwa Aliens walikuwepo duniani tangu enzi hizo kabla ya binadamu na hawajaondoka.
Si sehemu hizo pekee lakini wamekuwa wakitua maeneo mbalimbali duniani na kuna baadhi ya serikali duniani zinawajua.
Wataalam wa anga wanadai Aliens wako mbali kimaendeleo na wanafanya wanavyotaka.

No comments:

Post a Comment

advertise here