Friday, 17 July 2015

HABARI YA MJINI CHANZO CHA WEMA KUGOMBE UBUNGE CHAJULIKANA

LAYIII
Erick Evarist
MADAM Wema Sepetu ameweka bayana kuwa mtu aliyemsukuma kujiingiza kwenye siasa ni marehemu baba yake, Abraham Sepetu. Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Wema ambaye juzi alitarajiwa kuchukua fomu ya Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, alisema marehemu baba yake alimpa wazo hilo
Wema-Sepetu-akina-na-mama-yakeWema Sepetu na Mama yake.
Erick Evarist
MADAM Wema Sepetu ameweka bayana kuwa mtu aliyemsukuma kujiingiza kwenye siasa ni marehemu baba yake, Abraham Sepetu.
Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni, Wema ambaye juzi alitarajiwa kuchukua fomu ya Ubunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, alisema marehemu baba yake alimpa wazo hilo miaka mitano iliyopita.
wemasepetuWema Sepetu ‘Madam’ katika pozi.
“Marehemu baba aliniambia kwa nini usifanye siasa? Kwa nini usiwe kiongozi ambaye utawasaidia watu? Mwanzoni niliona ni vigumu lakini mwaka huu wa uchaguzi nimeona ni muafaka kwangu kuingia kwenye siasa,” alisema Wema.
Kwenye ubunge huo wa Viti Maalum mkoani Singida, Wema anatarajia kuwania nafasi hiyo kwa tiketi ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) akiwania nafasi mbili ambazo kwa sasa zinatetewa na Martha Mlata na Diana Chilolo.
Wema ambaye amefanya mambo mengi ya kijamii mkoani humo kabla ya kupata wazo la kuwania kiti hicho, ametajwa kuwa miongoni mwa wagombea watarajiwa waliopania kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili wanawake wa Singida.


No comments:

Post a Comment

advertise here