LAYIII
Msanii Bob Junior (kulia) akizungumza na Global TV Online kuhusiana na uzinduzi huo wa Video ya ‘Ndi ndi ndi’ ya Lady Jaydee.
Lady Jaydee akifanya mahojiano na baadhi ya wanahabari waliofika kwenye hafla hiyo.
VIDEO ya wimbo wa Lady Jaydee ‘Jide’ ya ‘Ndi ndi ndi’ imezinduliwa jana
rasmi jijini Dar es Salaam ambapo uzinduzi huo ulifanyika maeneo ya
Samaki Samaki-Masaki.
Katika hafla hiyo wasanii mbalimbali wa muziki akiwemo Bob Junior pamoja
na mashabiki wa muziki walihudhuria kumpa sapoti katika uzinduzi huo.
Akizungumza na Global TV Online, Bob Junior alianza kuipongeza video hiyo kwa kusema;
“Nimekuja hapa kumpa sapoti kama dada yangu na kama msanii mwenzangu.
Kiukweli video hii itafika mbali Afrika, kwanza ina ubora na pili
imefanywa na dairekta mkubwa Afrika (Justin Campos),” alisema Bob
Junior.
Video ya wimbo huo inatarajiwa kuanza kuonekana leo kupitia kipindi cha Friday Night Live kinachorushwa kupitia EATV.
No comments:
Post a Comment