LAYIII
Legendary wa muziki Marekani na Duniani Prince Rogers Nelson,
mwenye umri wa miaka 57 ambaye aliwahi kuuza takriban albamu milioni
100 na aliwahi kubuni chapa yake binafsi ya muziki uliokuwa na sauti na
ala za mchanganyiko wa muziki wa Rock na funk.
Asubuhi ya April 21 2016 Prince
amepatikana amefariki dunia katika makazi yake ya huko
Minneapolis, taarifa zinasema amekutwa amekwama kwenye lifti katika
studio Paisley Park, imeripotiwa kuwa staa huyo inawezekana alikuwa
anaumwa kwa kipindi cha muda mrefu ambako kulipelekea hata
kulazimika
kukatiza Show zake kutokana na kudhohofika kwa afya yake.
Imeripotiwa kwamba wiki iliyopita Staa huyo wa ‘Purple Rain’
alikuwa akirudi nyumbani kutoka kwenye show Antlanta Georgia ambapo
alilazimisha ndege yake binafsi kutua kwa dharura Molina na alipelekwa
hospitali jirani na gari la wagonjwa ambapo alitibiwa na kuruhusiwa
masaa machache baadae.
Prince aliwahi kushinda Tuzo za Grammy
saba, nyimbo zake tano ziliongoza chart na zingine 14 ziliingia Top 10
pia alishinda Oscar, best original song ‘Purple Rain’
PURPLE RAIN, UNAWEZA KUITAZAMA HAPA CHINI
No comments:
Post a Comment