Friday 22 April 2016

MTOTO MIAKA KUMI NA SITA AVUNJA RECORD KIKAO CHA UMOJA WA MATAIFA

LAYIII

Mtoto Mtanzania mwenye umri wa miaka 16 Getrude Clement kutokea Mwanza amehutubia mbele ya viongozi mbalimbali wa dunia kwenye mkutano wa umoja wa mataifa akiwa mwenye kujiamini na kutoonekana kuwa na hofu japo anaongea kwenye jukwaa ambalo linatazamwa na viongozi mbalimbali.
Mataifa zaidi ya 150 yalitia saini makubaliano ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ikiwemo Marekani ambapo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki moon ndio alimkaribisha Getrude kuongea kwa kusema ‘ni furaha yangu kumualika Getrude Clement ambaye pia ni mwakilishi wa vijana anayeishi Tanzania na anaziwakilisha sauti za vijana
Getrude alianza kwa kuwasalimia waalikwa huku ikiripotiwa Maraisi 60 walihudhuria na kisha akaeleza kuwawakilisha vijana na watoto ambapo alizungumzia mabadiliko ya tabia nchi, hatari yake na kwamba wamekua wakifikisha ujumbe kwa Wananchi juu ya mabadiliko hayo kama anavyoonekana kwenye hii video hapa chini.



Getrude

No comments:

Post a Comment

advertise here