LAYIII
Wakati wa vita ya kwanza ya dunia, serikali ya kijerumani ilitoa noti
za dharura ambazo zilikuwa ni za karatasi ya kawaida kabisa. Noti hizi
zilikuwa katika thamani za Rupie 1, 5, 10, 20, 50 and Rupie 200 ingawa
hizi za Rupie 200 zilikuwa adimu sana na sikufanikiwa kupata picha yake
Noti hizi za dharura zilikuwa hafifu sana na wakati mwingine zilikuwa
zinafyatuliwa kwa muhuri tu kama hii hapa chini ya Rupie 1.
Kwa muda mrefu fedha zilizotumia katika
nchi hii zilikuwa ni sarafu. Noti za karatsi zilianza kutumiaka mwaka
1905 wakati wa utawala wa mjerumani kwa upande wa bara. Noti hizo
zilitolweka katika thamani ya Rupie 5, 10, 50, 100 na rupie 500 kama
ionekanavyo hapa chini. Noti za rupie 500 zilikuwa chache sana na
sikufanikiwa kupata picha yake
Rupie 5..
Rupie 10...
Rupie 50..
Rupie 100..
Kwa upande wa zanzibar, mwaka huo huo
wa 1905, noti za Rupee za kizanzibari zilitolewa katika thamani za Rupee
5, 10, 20, 50, 100 na rupee 500 pia. Kwa bahati mbaya sikuweza kupata
picha zake zote, naonyesha mfano wa noti za rupee 5 tano tu
niliyofanikiwa kupata.
5 Zanzibari rupee...
1 rupee
5 rupee
10 rupee
20 rupee
50 rupee
1 rupee ikiwa imechakaa
Inaelekea kuwa mji wa Tabora ulikuwa na umuhimu wa pili kwa dar es
salaama wakati wa serikali ya kijerumani kwa vile unaonyeshwa katika
Noti zote. Kama mtakumbuka, ile sarafu ya dhahabu ya Rupie 15 ilikuwa
inaitwa "Tabora Pound."
No comments:
Post a Comment