LAYIII
Habari za siku rafiki na mpenzi msomaji wa DIRA YA MAFANIKIO, bila shaka
umzima wa afya na unaendelea vyema kujifunza ili kuboresha maisha yako.
Leo katika makala yetu napenda kukushirikisha namna unavyoweza kuipata
nguvu kubwa ya mafanikio utakayoweza kuitumia kuweza kutimiza malengo
yako makubwa.
Je, umeshawahi kujiuliza nguvu kubwa ya mafanikio inapatikana wapi? Hili ni swali muhimu sana kwako kwa sababu kuna wakati katika maisha, kwa sababu ya changamoto mbalimbali huwa tunajikuta tunakosa nguvu na mwelekeo wa kusonga mbele na kushindwa kujua tufanye nini? Inapofika hali hii, wengi hukata tamaa na kusahau kuitumia nguvu kubwa ya mafanikio waliyonayo kuwafanikisha.
Kama hali hii imekukuta huna haja ya kukata tamaa tena, unaweza kutumia nguvu hii kubwa uliyonayo kukufanikisha. Je, unajajua nguvu hii inapatikanaje hadi kukufanikisha? Sikiliza, mafanikio yoyote unayoyatafuta yapo Kwenye Kuanza. Kama kuna jambo unataka kulifanikisha ni lazima ulianze na sio kulisubiria. Nguvu kubwa ya kuendelea na kusonga mbele inapatikana kwa kuanza. Unapokuwa unaanza jambo, sio tu unakuwa na nguvu ya kuweza kulifanya bali nguvu hiyo inakuwa inaongozeka siku hadi siku.
CHUKUA HATUA MARA MOJA ILI KUFANIKIWA.
Moja kati ya wanasayansi waliopata kuwepo katika hii dunia, Isack Newton aliwahi kulieleza hili vizuri katika sheria yake ya mwendo kwamba kitu chochote kikiwa kwenye mwendo kitaendelea kuwa kwenye mwendo huo na kitu chochote ambacho kipo katika hali ya kutulia au utulivu, kitaendelea kutulia siku zote mpaka itokee nguvu nje ya hapo ya kubadili hali hizo.
Tafsiri au maana yake ni nini hapa? Ni kwamba kama utaamua kuchukua hatua juu ya maisha yako, utazidi kupata nguvu ya kukufanikisha kwenye mafanikio unayoyahitaji. Chochote unachotaka kukifanya kwenye maisha yako hata kiwe kikubwa vipi, siri kubwa ya kukifanikisha ipo kwenye kuanza.
Mafanikio yote makubwa chini ya jua yalianza kwa kufanya kwanza na sio kusubiri. Kumbuka ”DO THE THINGS YOU WILL HAVE THE POWER TO ACCOMPLISH IT.” Kama kuna jambo unataka kulifanya, wewe lifanye tu acha kujiandaa sana, wala kusubiri sana kwani nguvu ya kufanikisha jambo hilo itapatikana wakati unafanya. Kama ni uzoefu mkubwa utaupata kwa kuanza. Hivi ndivyo mafanikio makubwa yanavyopatikana kwa kuchukua hatua za utekelezaji.
Tumia kanuni hii bora ikusaidie kufanikiwa kwa viwango vya juu, kumbuka siku zote unalo jukumu la kuhakikisha unakuwa bora kila siku.

No comments:
Post a Comment