layiii
MAPACHA wa muziki wa R&B wa Nigeria, Peter na
Paul Okoye wanaounda kundi la P-Square, wamesema hawataki kuitwa
wanenguaji, bali waitwe waburudishaji.
Wasanii
hao ambao hivi sasa wanachukuliwa kuwa waimbaji bora zaidi barani
Afrika, wamesema wanajisikia vibaya kuitwa wanenguaji, kwani kuna mambo
mengi wanayoyafanya katika tasnia ya muziki.“Nimezoea kuwasikia watu
wakisema nawapenda P-Square kwani wanajua kucheza, lakini ukweli ni
kwamba huwa sipendi watu watuite wanenguaji.
“Ni vyema wakatuelezea kuwa sisi ni waburudishaji na wanamuziki kwani hivyo ni vizuri zaidi,” alisema Peter na kuongeza kwamba nyimbo za mapenzi hivi sasa hazina masoko sana nchini Nigeria kama baadhi ya mashabiki wanavyodai, akisema nyimbo za mapenzi ambazo ziliwahi kuwika sana ni ‘Olufunmi’ wa Styl Plus na ‘Beautiful Onyiye’ wa P-Square.
“Hivi sasa nyimbo za mapenzi hazina soko kwani ni za kizazi kingine. Hata hivyo, kwa vile bado kuna mashabiki kadhaa wanazipenda, tutazifufua, alimalizia akijibu hoja ya shabiki mmoja aliyemwambia anapenda kuzisikiliza nyimbo zao za mapenzi.

No comments:
Post a Comment