LAYIII
Klabu za Ligi Kuu soka Tanzania bara bado hazijakidhi vigezo vya kupata leseni ya kudumu ya vilabu, kupitia kwa mkuu wa idara ya habari wa shirikisho hilo Baraka Kizuguto amethibitisha vilabu vingi kushindwa kupata leseni za vilabu isipokuwa klabu ya Azam FC na Mtibwa Sugar.
Vilabu 14 vinavyoshiriki Ligi Kuu Tanzania
bara vimeshindwa kukidhi vigezo vya kupata leseni za kudumu na kupewa
leseni za muda kwa kipindi cha miezi sita ili viweze kutimiza vigezo
hivyo na kuweza kupata leseni hiyo, vilabu vinavyotajwa kutimiza vigezo
kwa asilimia 95 ni Azam FC pamoja na Mtibwa Sugar ambavyo vinamiliki viwanja vyao.
“Vilabu
vya Ligi Kuu kwa asilimia 95 hadi 97 hawajatimiza vigezo vya kupata
leseni ya vilabu ukiondoa vilabu vya Azam FC na Mtibwa Sugar ambao wana
viwanja vyao hawa wamekidhi vigezo vya kupata leseni kwa asilimia 95,
kilichofanyika ni kuwa kamati ya sheria na hadhi za wachezaji imetoa
leseni ya muda wa miezi 6 kwa timu zote za Ligi Kuu ili kutimiza vigezo
vya kupata leseni”>>> Baraka Kizuguto
Hii ni sauti ya Baraka Kizuguto
No comments:
Post a Comment