LAYIII....
Unaweza uka bonyeza play kumsikiliza Steve Nyerere
Ni stori ya kisiasa ambayo ilianza
kuchukua headlines kwenye mitandao mbalimbali kuhusu wasanii wawili wa
Bongo Movies, Aunt Ezekiel na Vicent Kigosi aka Ray kuondoka UKAWA na
kuhamia chama cha Mapinduzi.
Baada ya taarifa hizo kuchukua nafasi
kubwa kwenye mitandao sasa ripota wa millardayo.com amezungumza na
Steve Nyerere ambaye ni mwenyekiti wa kampeni ya Mama ongea na Mwanao…’Ndugu
zetu wakina Vicent Kigosi na Aunt Ezekiel walitoroka wamerudi CCM
kabla hawajatangaza lakini watatangaza wamerudi kwa kishindo kikubwa
wanaamini bila hapo walipofika bila nguvu ya Mh Jakaya Mrisho Kikwete
wasingiweza kufika‘ – Steve Nyerere
‘Kwa hiyo nataka kuwaambia watanzania
kuwa hao watu wamerudi katika chama cha mapinduzi na wala msidanganywe
pilika pilika za huku na kule hawa watu ni wanachama wa CCM hai
walitoroka na sifa ya kutoroka ni kukosa nidhani kwa sisi wazazi ambao
tuna watoto , mtoto akitoroka unatakiwa umpe adhabu ili siku nyingi
afahamu njia ya sahihi na njia sahihi ni chama cha Mapinduzi ambacho
kina Dkt John Pombe Magufuli na Mama Samia Suluhu’ – Steve NyerereUnaweza uka bonyeza play kumsikiliza Steve Nyerere
No comments:
Post a Comment