LAYIII
Baada ya kuachana na mchumba wake miaka miwili iliyopita mwimbaji wa R&B Christina Milian alianza kuonekana sana na rapper Lil Wayne baada
ya kujiunga na lebo ya msanii huyo, muda mfupi
badaae wawili hao
wakaingia kwenye mahusiano ya kimapenzi na mpaka sasa wana zaidi ya
mwaka mmoja pamoja.
Lakini leo headlines za wawili hawa ni
tofauti kidogo… wapenzi hao wamethibitisha kuwa wameachana toka mwezi
uliopita lakni waliamua kukaa kimya kwanza na kuweka baadhi ya mambo yao
sawa kabla ya kutangaza kwa watu kuwa uhusiano wao wa kimapenzi
umeisha.
Msemaji wa karibu wa watu hao anasema sababu kubwa iliyopelekea kuachana kwao zinatokana na ratiba za wawili hao kubana sana.
>>>“Wanaachana
sio kwamba wanapenda ila ratiba zao zinawabana sana, wanakosa muda wa
kuonana na kuwa pamoja, Lil Wayne anafanya sana tour za wasanii wake na
za kwake pia na pia anaifanyia kazi album ya Christina Milian… isitoshe
hata Christina Milian ana mambo mengi, vipindi vya TV, Talk Shows za
kuandaa na vingine vingi, so wameona bora waachane lakini sio kwa sababu
wamechokana ila ratiba za kazi haziwapi muda wa kutosha kuwa pamoja”. <<< Alisema msemaji wa karibu wa mastaa hao.
No comments:
Post a Comment