Friday, 24 July 2015

ASABABISHA MAUAJI KTK NYUMBA YA SINEMA NAYE AJITUNDIKA

LAYIII
Masaa machache yaliyopita kumetokea tukio la mauwaji Marekani ambako mwanaume mmoja aliamua kupiga risasi ovyo akiwa kwenye nyumba ya Sinema iliyopo jijini Lafayette Louisiana na kusababisha vifo vya watu 2 na majeruhi ya watu 9 kabla ya kujiua yeye mwenyewe.

cinema5

Tukio hilo limewashituka na kuwatisha watu wengi ambao wanadai hawaoni wala hakukuwa na sababu ya mtu huyo kufanya hicho alichokifanya kwenye eneo hilo.
cinema
Mwanaume huyo ambaye jina lake halijafahamika alikuwa na umri wa miaka 58 na kutokana na ushuhuda wa wafanyakazi wa eneo hilo la sinema alikuwa ni mhudhuriaji mzuri wa sehemu hiyo mara kwa mara.
Polisi wanaendelea na upelelezi juu yake huku wakifanya jitihada ya kumtabua yeye ni nani na kuwatafuta wanafamilia wake.
cinema4
Polisi wanasema karibia watu 100 walikuwemo ndami ya sehemu hiyo ya sinema kwa ajili ya kuangalia movie mpya ya Comedy “Trainwreck” kabla ya risasi hizo kupigwa ovyo.
Tukio hilo lilitokea kwenye mida ya saa 8:30 usiku jijini Lafayette Louisiana Marekani.

No comments:

Post a Comment

advertise here