LAYIII
Ni Obama kila kona! Muda wowote kuanzia leo wananchi wa Kenya
watashuhudia kutua kwa Rais wa Marekani, Barack Hussein Obama, nchini
humo huku stori kubwa ikiwa ni ulinzi uliowekwa kwa hofu ya kundi
‘haramu’ la ugaidi la Alshabaab, Ijumaa linakupeleka hadi kwa majirani
zetu hao.
Ziara ya Obama ambaye ana asili ya Kenya kutokana na baba yake, Hussein
Obama kuwa ni raia wa Kenya, itakuwa na ulinzi ambao hata mwenyeji wake,
Rais Uhuru Kenyatta hana.
VIKOSI VYA ULINZI
Habari kutoka nchini humo zilidadavua kwamba, vikosi vya ulinzi vya
Marekani, CIA, FBI na kile cha siri cha Secret Service vilitua nchini
humo miezi kadhaa na kuungana na majeshi ya Kenya ili kuweka mambo safi.
Meli iliyobeba ndege za kivita.
MANOWARI ZA KIVITA
Ilielezwa kwamba, meli na manowari za kivita vimepiga kambi eneo lote la
pwani ya nchi hiyo katika Bahari ya Hindi, lengo likiwa ni kuimarisha
usalama wa kiongozi huyo mkubwa duniani pamoja na jopo la
wafanyabiashara atakaoandamana nao.
B52 YAEGESHWA PWANI
Ilielezwa kwamba, jeshi la kwenye maji la Marekani limejikita Bahari ya
Hindi kwenye ukanda wote wa Afrika Mashariki kujiandaa kuzuia shambulizi
la kivita wakiwa na silaha nzito ndani ya ndege ya B52 ambayo
imeegeshwa pwani ya nchi hiyo.
KAMERA, SATELAITI ZAFUNGWA
Ilisemekana kwamba, Jeshi la Kenya wameweka doria kwenye Jiji la Nairobi
ambalo limetulia tuli huku likimulikwa kwa kamera maalum na satelaiti
za kijeshi, barabara kufanyiwa usafi na nyingine kufungwa huku bendera
za Kenya na Marekani zikiwa zimepamba Jiji la Nairobi.
AIR FORCE ONE
Imedadavuliwa kwamba, Obama atatua na ndege ya Rais wa Marekani ya Air
Force One aina ya Boeing 747-200B kisha atapokelewa na gari analotumia
Marekani ambalo lilitangulia kuwasili Kenya.
UWANJA WA NDEGE
Ilielezwa kwamba, kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta
atakaotua Obama, kumejaa ndege za Jeshi la Marekani na hauruhusiwi
kutumiwa na ndege nyingine za biashara.
Hali ndivyo ilivyo kwa viwanja vingine pamoja na bandari, hakuna
biashara inayoendelea hadi kiongozi huyo amalize ziara yake nchini humo.
Rais wa Marekani, Barach Obama (kushoto), mkewe Michelle Obama (kulia) na katikati ni Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
MAMLAKA YA ANGA
Ilielezwa kwamba, Mamlaka ya Anga ya Marekani na Makao Makuu ya Jeshi
hilo Pentagon wanafanya kazi kama siafu kuhakikisha anga lote lipo
shwari.
Kuna taarifa kwamba, wafanyakazi wote serikalini wasiohusika na usalama
na ziara hiyo watakuwa miguu atakapowasili Obama kwani hawataenda
kazini.
Kuhusiana na ulinzi wa Kenya, hata nchi za Tanzania, Somalia, Eritrea,
Uganda, Rwanda na Burundi nazo zinamulikwa kusije kukatokea lolote.
Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.
KILICHOMLETA
Akiwa nchini Kenya, Obama atafanya mkutano na Rais wa Kenya, Uhuru na
baada ya hapo wawili hao watahudhuria Kongamano la Ubunifu wa Kibiashara
Ulimwenguni la 2015 linalofanyika kwenye mji mkuu wa nchi hiyo,
Nairobi.
Hii itakuwa ziara ya tatu ya Obama Afrika baada ya mwanzo kutembelea Ghana, baadaye Senegal, Afrika Kusini na Tanzania.
Kikundi cha wapiganaji cha Al-shabaab.
MAUAJI YA AL-SHABAAB
Ulinzi huo umekuja kufuatia matukio ya mauaji ambayo yamekuwa yakifanywa
na Al-shabaab ambao walihusika na mauaji ya wanafunzi 148 katika Chuo
Kikuu cha Garissa na shambulizi la mwaka 2013 la Jengo la Biashara la
Westgate ambapo takriban watu 67 waliuawa.
Al-shabaab wamekuwa wakifanya mashambulizi ya mara kwa mara kwenye
maeneo mbalimbali ya Kenya yaliyo karibu na mpaka wa Somalia, wakidai
lazima vikosi vya Kenya viondoke nchini Somalia ndiyo maana Marekani
wameamua kuweka ulinzi mkali kuliko ule wa Tanzania alipotua Obama mwaka
2013.
KIJIJINI KOGELO
Wakati hayo yakiendelea, inaelezwa kwamba, wakazi wa kijiji anakotoka
mzazi wa Rais Obama, Kogelo, Magharibi mwa nchi hiyo, wanaamini kuwa
kiongozi huyo atawatembelea kijijini hapo hivyo kwao ni hatua kubwa
kwani atazidi kuwaboreshea maisha.
Kogelo ni kijiji kidogo alikozaliwa mzee Hussein Obama. Kijiji hicho
hakikuwa kikijulikana wala kuwa na huduma muhimu kama maji na umeme,
kama vijiji vingine nchini humo, hadi pale Barack Obama alipochaguliwa
kuwa seneta ambao mwaka 2006 alifika kijijini hapo na kusaidia mambo
mengi. Hivi sasa kijiji hicho kina umeme, barabara ya lami na shule.
Obama na Bibi yake.
KWA MARA YA KWANZA
Obama amepanga pia kutembelea Makao Makuu ya Umoja wa Afrika yaliyo
Addis Ababa, Ethiopia ikiwa ni ziara ya kwanza kwa Rais wa Marekani
kuzuru umoja huo tangu kuasisiwa kwake.
No comments:
Post a Comment