LAYIIIII

Magazeti
Ni kweli SITTA alikaata rushwa mil.140? Baba amchinja mwanaye wa mwaka 1 Dar, wimbo wa albino wamtoa chozi JK..#MAGAZETINI JUNE14
MWANANCHI
Makada wa CCM waliotangaza nia au
kuchukua fomu za kuomba kupitishwa na chama hicho kuwania urais,
wameeleza jinsi rushwa, ufisadi na udhaifu katika ukusanyaji kodi huku
wakijinadi kuwa wao ndiyo wataondoa uovu huo iwapo watapitishwa kushika
nafasi hiyo ya juu kisiasa.
Lakini hakuna hata mmoja aliyeiponda
Serikali kwa kushindwa kudhibiti rushwa, ambayo baadhi walishasema kuwa
imekithiri hata kwenye chama hicho tawala, huku mmoja akisema kuwa iwapo
CCM itampitisha mlarushwa, atajiondoa.
Kati ya waliotangaza nia na kuchukua
fomu, makada 11 ni mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne wakiwamo
mawaziri waandamizi walioshika nafasi za juu na waliofanya kazi katika
awamu zote nne.
Pia wamo makada waliokuwamo kwenye
Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Nne, lakini wakaondoka kwa
sababu tofauti, huku kundi jingine likihusisha watendaji wakuu wa zamani
wa Idara ya Usalama wa Taifa.