Sunday 14 June 2015

MAKALA YA SIASA SITTA AKATAA MIL 140 JE NI ZA NINI KIPI KIMEFUATA ,,,,,,,?KILICHO FUATA STORY NYINGINE

LAYIIIII

Magazeti

Ni kweli SITTA alikaata rushwa mil.140? Baba amchinja mwanaye wa mwaka 1 Dar, wimbo wa albino wamtoa chozi JK..#MAGAZETINI JUNE14

LEEE
MWANANCHI
Makada wa CCM waliotangaza nia au kuchukua fomu za kuomba kupitishwa na chama hicho kuwania urais, wameeleza jinsi rushwa, ufisadi na udhaifu katika ukusanyaji kodi huku wakijinadi kuwa wao ndiyo wataondoa uovu huo iwapo watapitishwa kushika nafasi hiyo ya juu kisiasa.
Lakini hakuna hata mmoja aliyeiponda Serikali kwa kushindwa kudhibiti rushwa, ambayo baadhi walishasema kuwa imekithiri hata kwenye chama hicho tawala, huku mmoja akisema kuwa iwapo CCM itampitisha mlarushwa, atajiondoa.
Kati ya waliotangaza nia na kuchukua fomu, makada 11 ni mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Nne wakiwamo mawaziri waandamizi walioshika nafasi za juu na waliofanya kazi katika awamu zote nne.
Pia wamo makada waliokuwamo kwenye Baraza la Mawaziri la Serikali ya Awamu ya Nne, lakini wakaondoka kwa sababu tofauti, huku kundi jingine likihusisha watendaji wakuu wa zamani wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Lakini bado tatizo hilo la rushwa limekuwa likitumiwa na makada hao wa CCM wanaowania urais wakati wakijinadi kwa wanachama wao kwamba watafumua mfumo uliopo, kusuka upya sheria na kuimarisha taasisi za fedha ili watuhumiwa wakubwa wa rushwa wafikishwe kortini na kufungwa, badala ya kuwakamata walarushwa wadogowadogo pekee.
Kwa mfano, akitangaza nia ya kuwania urais kijijini kwao Butiama, Charles Makongoro ambaye ni mtoto wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, alisema anaomba kibali cha kuisaidia CCM ikomeshe rushwa, na atakapoingia madarakani, ili asiwaangushe Watanzania, anahitaji chama imara kisicho na shaka kama ilivyo sasa.
Kosa la Rais Jakaya Kikwete ni kuwapenda sana marafiki zake. Kwa bahati mbaya, baadhi ya marafiki zake hao ni vibaka,” alisema Makongoro ambaye ni mbunge wa Afrika Mashariki.
Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe aliwaambia wafuasi wake mkoani Lindi kwamba ili kutekeleza utawala bora, hawezi kukaa kimya kuona rushwa, ubadhirifu, ufisadi vikichukua nafasi katika utawala wake.
“Ninawatumia salamu mapema, sitakuwa na kigugumizi kwa wanaotesa Watanzania. Nitahakikisha Watanzania wanachukia rushwa na kutakuwa na sheria kali dhidi ya mtoa na mpokeaji rushwa. Kama ni watumishi wa umma, watakwenda na maji…,
Ahadi ya kukomesha rushwa pia ilitolewa na Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta aliyesema kwamba anataka kulifanyia Taifa mambo matano, ikiwa ni pamoja na kutenganisha biashara na siasa na kusimamia maadili ya viongozi wa umma.
“Ili kukomesha tatizo la rushwa, hatuna budi kutunga sheria itakayotenganisha biashara na uongozi,” alisema Sitta kwenye Ikulu ya Wanyanyembe iliyopo Itetemia, Tabora.
MWANANCHI
Waziri wa Uchukuzi, Samuel Sitta amesema anasimama kifua mbele kupambana na rushwa kwa kuwa aliwahi kuikataa rushwa ya Dola 70,000 (sawa na Sh140,000) milioni).
Sitta alisema kuna baadhi ya watia nia wanaopita wakisema kuwa wakiwa marais watapambana na rushwa wakati ukiwatazama macho yao yanaonyesha ni wala rushwa.
“Nilitumwa Canada kutafuta ndege tatu, jioni moja tukiwa Canada tunajiandaa kuondoka, akaja mkurugenzi wa masoko wa kampuni tuliyonunua ndege, akaniambia waziri tuna kautaratibu hapa ukifanikisha ndege zetu zikanunuliwa tunatoa bakshishi ya Dola 70,000 utataka hizi hela tuzipeleke benki gani,” alisema Sitta akimnukuu ofisa huyo wa masoko.
“Watazameni hawa watu… mtu kawa waziri mwaka mmoja leo anataka urais, halafu anasema atapambana na rushwa…utapambana na rushwa wapi wakati hata hujapita kwenye mitego ya rushwa. Watazameni kwa makini, mtawajua tu kwa macho, kwani macho yao yamekaa kijanjajanja kweli,” alisema. Aliendelea, “Kwa kuwa mimi nililelewa vizuri nilijua tu huo ni mtego wa shetani, nikamwambia mkurugenzi nitampa jibu kesho, nikawasiliana na wakubwa zangu kwanza wakakubali ni chukue hiyo pesa ikasomeshe marubani wa ndege.”
Sitta aliwataka wananchi hao kuwatazama kwa makini watangaza nia hao, na kuwauliza iwapo tayari walishawahi kupambanishwa na rushwa.
Wakazi wa Kigoma wametakiwa kuwa makini na kauli za baadhi ya viongozi wa Serikali wanaojinadi kwa kusema wanawapenda Watanzania maskini, lakini mioyoni mwao hawana huruma.
Akiwa katika ofisi ya CCM mkoa, Katibu wa CCM Wilaya ya Kigoma Mjini, Nohoji Kubaji alimkabidhi Lowassa fomu 45 za wana CCM waliomdhamini.
“Wapo viongozi, wanajifanya wanawapenda na kuwajali watu masikini, lakini wao wenyewe unawakuta ni matajiri, hawa jamaa ni waongo sana hawa,”.
Lowassa aliwataka wakazi Kigoma kumuombea ili dua na sala zao ziweze kumsaidia afikie malengo aliyojiwekea. “Nina dhamira ya kuwatumikia, lakini lazima mniombee sana dua na sala ili mambo yangu yaende vizuri hatimaye nishinde kuwa Rais wa Tanzania. Mimi nachukia sana umaskini, kwa hiyo lazima tuwe kama Malaysia ambayo kiongozi wake alipambana kuhakikisha wananchi wanaondokana na umaskini,”.
MWANANCHI
Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad ameitaka CCM kujiandaa kisaikolojia kukabidhi madaraka kwa chama chake baada ya Oktoba, akisema katika chama chake hakutakuwa na neno “kushindwa”.
Maalim Seif, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, aliwataka vijana popote walipo kujiandikisha kwa ajili ya uchaguzi ili kujitayarisha na ushindi aliouita mkubwa.
“Hakuna kushindwa CUF, kwa hivyo mawazo yenu yawe na kushinda tu. Vijana, hakuna kukaa ukasema ushamaliza kupiga kura, unakwenda kwako unasubiri ushindi. Hakuna hilo mwaka huu, lazima mjitahidi kulinda ushindi wenu,”  Maalim Seif.
 Katibu huyo wa CUF alisema wananchi wa Pemba walioko Arusha, Mwanza na sehemu nyingine warudi kujiandikisha kwenye Daftari la Wapigakura na kuwataka kutoacha fursa hiyo ambayo ni haki yao ya kidemokrasia.
Akitilia mkazo suala hilo, aliyekuwa waziri wa SMZ, Mansoor Yussuf Himid alimtaka Maalim Seif baada ya kupiga kura yake kurudi nyumbani na kuwaachia vijana kumkabidhi ushindi wa chama hicho.
Mansoor alisema hatima ya ushindi wa Zanzibar ipo mikononi mwa vijana, hivyo wanapaswa kuhakikisha ushindi wa Zanzibar unapatikana katika ya mikono yao.
Akihutubia mkutano huo, Mwanasiasa Hassan Nassor Moyo alisema kazi ya Maalim Seif na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Amani Abeid Karume kuleta umoja wa kitaifa si jambo jipya kwa kuwa lilianzia kwa Mzee Karume ambaye alitunga sheria kuondosha ubaguzi na kuwaweka wananchi wote wa Zanzibar kuwa kitu kimoja.
Katika hotuba yake ya takriban saa moja iliyorushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha Star TV, Maalim Seif alisema Maalim Seif alisisitiza nia yake ya kuifanya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili ili iondokane na adhabu ambazo siyo stahiki kwake.
MWANANCHI
Rais Jakaya Kikwete ametokwa na machozi wakati akisikiliza wimbo ya masikitiko ya watoto wenye ulemavu wa ngozi (albino), na akaeleza kuwa ni upumbavu kuamini kuwa viungo vyao vinaleta utajiri.
Rais Kikwete alisema mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi yanayoendelea nchini yanamsononesha na kulitia doa Taifa.
Rais Kikwete alisema wimbo wa watoto wenye albino kutoka Tanga, ulivyoanza alianza kuhisi angetokwa machozi na baadaye alishindwa kujizuia na kutokwa na machozi.
Hawa watoto wameimba mambo ambayo yamenigusa sana, na tumepokea kilio chenu kwa umuhimu mkubwa na ninaahidi tutashirikiana kuyashughulikia matatizo yenu,” alisema.
Alisema suala la matibabu ya albino ni jambo ambalo linashughulikiwa, ili kuhakikisha vifaa tiba ambavyo vinahitajika hasa kutibu magonjwa ya ngozi vinapatikana na kuwawezesha kupata matibabu bure.
Akizungumzia hatua za Serikali, Rais Kikwete alimpa nafasi Waziri wa Mambo ya Ndani, Mathias Chikawe kueleza hatua zilizofikiwa katika kuunda kamati ya kitaifa ya kuishauri Serikali.
Waziri Chikawe alieleza kuwa tayari wizara yake, imekamilisha mchakato wa kuunda kamati hiyo, ambayo itakuwa na wajumbe 15, watano kutoka chama cha wenye albino, watano chama cha waganga wa jadi na watano kutoka serikalini.
Awali Mwakilishi ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNICEF) nchini, Zulmira Rodrigues aliiomba Serikali kuwaondoa watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) waliowekwa katika vituo maalumu, kwa kuwa kitendo hicho kinawanyanyapaa.
Akizungumza katika mkutano uliokuwa wa kuelezea maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uelimishaji kuhusu albino jijini hapa jana, Rodrigues alisema vituo hivyo vinaweza kutumika kwa ajili ya kuwahifadhi albino kwa muda mfupi na si kuvifanya suluhisho la kudumu litakalowapa ulinzi.
MTANZANIA
Baba mmoja anayetajwa kwa jina la Maneno Kasugu anadaiwa kumchinja hadi kufa mtoto wake mwenye umri wa mwaka .
Kasugu ambaye anaelezwa kuwa ni mlinzi, anadaiwa kutekeleza kitendo hicho cha kinyama jana saa 4 asubuhi eneo la Mabibo Loyola Jijini Dar es salaam baada ya kumteka mtoto wake huyo aliyekuwa akiishi na bibi yake mzaa mama.
Bibi huyo Mwanaidi Hassan ambaye alikua akishi na mjuu wake huyo hadi mauti inamkuta alisema alieleza sababu mbili ambazo anadhani huemda zimechangia kifo cha mjuu wake.
Alidai Kasugu na mkewe walikua na ugomvi na pia kushindwa kutumia kiasi cha shilingi 50,000 alizotoka mkwe wake huyo baada ya kumteka mtoto.
Kwa mujibu wa bibi huyo Kasugu alifika nyumbani hapo saa mbili asubuhi na kisha kumchukua mtoto bila taarifa.
“Mimi nilikua bado nimelala, mama wa mtoto alikua chumbani kwake na mtoto alikua anacheza, alipofika akamchukua mtoto na kuandoka”.
Anasema baada ya muda kupita bila mtoto kuonekana ndipo mama wa mtoto alipoamua kumpigia Kasugu simu kutaka kufahamu na kutaka atumiwe 50,000 ili awaeleze mtoto alipo na tofauti na hapo asingeonekana.
Baada ya muda watu walidai kukuta mwili wa mtoto aliyechinjwa ukiwa nyuma ya shule ya Loyola na ndipo walipotoa taarifa kituo cha polisi cha urafiki ambao wlaifika na kuuchua mwili wa mtoto huyo.
NYAKATI
Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amewataka Watanzania kumuombea sana kwa Mungu ili chama chake kiweze kumchagua kuwa Rais kwani amejiandaa kuipeleka nchi katika mchakamchaka wa maendeleo.
Pia amesema akifanikiwa kuwa Rais atamwaga milioni 500 kwa kila kata kwa ajili ya shughuli za kimaendeleo.
Alisema wachimbaji wadogowado wa madini watapewa mikopo ili kuwawezesha kujiimarisha katika shughuli zao za uchimbaji wa madini.
Alisema yeye anawapenda sana Watanzania hali iliyomfanya achukue uamuzi wa kugombea kutokana na kuguswa na hali ya umaskini wa wananchi wenzake.
Alisema ili kuwakomboa wananchi kama watampa ridhaa ya kuwaongoza, ataifikisha Tanzania pazuri.

 


No comments:

Post a Comment

advertise here