Thursday, 11 June 2015

MWANARIHADHA MLEMAVU OSCAR PISTORIUS KUACHIWA MWEZI AGOSTI

NA LAYIIII ON SPOT
Oscar Pistorius akilia wakati wa hukumu yake.
MWANARIADHA maarufu nchini Afrika Kusini ambaye ni mlemavu, Oscar Pistorius huenda akaachiwa huru mwezi Agosti, mwaka huu baada ya kukaa jela kwa miezi 10.


Pistorius akiwa katika mashindano ya riadha.
Mwanariadha huyo anatumikia kifungo cha miaka mitano baada ya kukutwa na hatia ya kumuua kwa kumpiga risasi mpenzi wake ambaye alikuwa mwanamitindo aitwaye Reeva Steenkamp.
"Oscar anaweza kuachiwa huru mwishoni mwa mwezi Agosti," mmoja wa wanafamilia wa staa huyo ambaye hakutaka kutaja jina lake aliliambia Shirika la Habari la Reuters.
Pistorius alianza kutumikia adhabu yake ya miaka mitano Oktoba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

advertise here