LAYIII
Usafiri wa anga japo kumekuwa na Ripoti
mfululizo kuhusu ajali za ndege lakini bado, usafiri wa anga unaendelea
kuwa usafiri salama zaidi Duniani.
Sheria, kanuni na taratibu za usafiri wa
anga zinafanya pia usafiri huo kuendelea kuwa salama zaidi, watu
hawataki kabisa Rubani alete utani kwenye kazi !!
Rubani mmoja wa Kampuni ya Air Baltic
pamoja na wenzake watatu walilewa pombe kama saa nne kabla ya kuanza
safari na ndege ya abiria ambayo ilikuwa na abiria kama 100 hivi kutoka
Norway, walipogundua kafanya kosa hilo walimzuia asiruke na ndege hiyo
na ishu ikapelekwa Mahakamani.
Rubani huyo pamoja na wafanyakazi
wenzake wengine wawili wamekiri Mahakamani kufanya kosa hilo, Mahakama
imempa kifungo cha miezi sita jela alafu wenzake ambao ni wahudumu wa
kwenye ndege hiyo mmoja amehukumiwa kifungo cha siku 45 mwingine siku
60.
No comments:
Post a Comment