Monday 13 July 2015

MJUE MAGUFULI MGOMBEA URAIS CCM HAPA

LAYIII

- Alizaliwa Oktoba 29, 1959 wilayani Chato, wakati huo ikiwa ni sehemu ya mkoa wa Kagera (sasa mkoa wa Geita).
- Mwaka 2006 – 2009, Shahada ya Uzamivu ya Kemia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
- Mwaka 1991 – 1994, Shahada ya Uzamili ya Kemia katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na baadaye Chuo Kikuu  cha Salford, Uingereza.
- Mwaka 1985 – 1988, alisoma Shahada ya Kwanza ya Elimu katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.

- Mwaka 1981 – 1982, alisoma diploma katika Chuo cha Mkwawa akichukua masomo ya Kemia na Hisabati.
- Mwaka 1979 – 1981, alipata elimu ya juu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Mkwawa, Iringa.
- Mwaka 1977 – 1978, alisoma elimu ya sekondari katika Shule ya Sekondari Lake, Mwanza.
- Mwaka 1975 – 1977, alisoma Shule ya Msingi Katoke, Biharamulo mkoani Kagera.
- Mwaka 1967 – 1974, alisoma Shule ya Msingi, Chato.
- Machi 1984 – Juni 1984 alihudhuria mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Mpwapwa mkoani Dodoma.
- Januari 1984 – Machi 1984 alikuwa JKT Makuyuni, Arusha.
- Julai 1983 – Desemba 1983 alikuwa JKT Makutupora, Dodoma.
UZOEFU
- Mwaka 2010 – hadi sasa: Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Chato.
- Mwaka 2008 – 2010: Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi; Mbunge wa Biharamulo Mashariki (Chato).
- Mwaka 2005 – 2008: Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki      (Chato)
- Mwaka 2000 – 2005: Waziri wa Ujenzi, na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
- Mwaka 1995 – 2000: Naibu Waziri wa Ujenzi; na Mbunge wa Biharamulo Mashariki.
- Mwaka 1989 – 1995: Mkemia Chama cha Ushirika cha Nyanza Cooperative Union (Ltd.), Mwanza.
- Mwaka 1982 – 1983: Mwalimu Shule ya Sekondari Sengerema (akifundisha masomo ya Kemia na Hisabati).
- Amewahi kutwaa tuzo mbalimbali za ndani na nje ya nchi.
- Ameshiriki na kuongoza mikutano mingi ya kitaifa na kimataifa.
- Ameoa na ana watoto kadhaa.
- Ameandika vitabu na majarida mbalimbali. Baadhi ya machapisho aliyoshiriki ni “Securing the Mechanism of the    Decomposition of CaCO3 by the Thermodynamics of the Reaction” na “A New Rate Equation for Solid State  Decompositions and its application to the Decomposition of CaCo3”.
CREDIT: NIPASHE

No comments:

Post a Comment

advertise here