Monday 13 July 2015

LOWASSA GUMZO KILA KONA, KAGUFU HAIJAWAI TOKEA

LAYIII
Mwandishi Wetu
NIJohn Pombe Joseph Magufuli ambaye amepita kwa kishindo na ‘usimpimie’ kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan, lakini yaliyojiri katika mchakato wa kumpata mgombea huyo, hayajawahi kutokea, Ijumaa Wikienda limechimba na kuchimbua.
Mwandishi Wetu
NIJohn Pombe Joseph Magufuli ambaye amepita kwa kishindo na ‘usimpimie’ kuwa mgombea urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan,
lakini yaliyojiri katika mchakato wa kumpata mgombea huyo, hayajawahi kutokea, Ijumaa Wikienda limechimba na kuchimbua.
Mh.John Pombe Joseph Magufuli akiwashukuru wajumbe baada ya kumteua kuwa mgombea wa CCM.
Sarakasi zilikuwa ni nyingi lakini katika kukiokoa chama kisizame mjini Dodoma, ilibidi kutumia akili nyingi na nguvu ya ziada kumpata mtu clean (safi) ambaye ni Magufuli.
Uchunguzi wa kina uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba, tangu uhuru wa Tanzania (1961) hakujawahi kuwa na mvutano mkubwa, ikiwemo wajumbe kuonesha upinzani dhahiri mbele ya mwanyekiti wao wakati wa mikutano ya chama hicho katika kumchagua mgombea achilia mbali idadi kubwa ya waliojitokeza.
Baadhi ya wapiga kura waliozungumza na gazeti hili walisema, mwaka huu uchaguzi ndani ya CCM umekuwa mgumu kiasi kwamba, hakuna rekodi yoyote inayofanana nayo hapo miaka ya nyuma.

Akitoa neno baada ya kuteuliwa.
“Mimi nimekuwepo tangu uhuru, sijawahi kuona ugumu wa uchaguzi ndani ya chama, tangu Tanu (Tanganyika African  National Union) mpaka sasa CCM. Hii ni hali ya hatari.“Kwanza hata wajumbe wenyewe walikosa adabu hata kwa mwenyekiti wao,” alisema mzee Bakar Masoud, mkazi wa Msasani, Dar.
“Watu wanabebana bwana! Mimi sijawahi kuona, safari hii sijui haya mambo yametokea wapi?” alisikika mwanachama mmoja wa chama hicho akisema kutokea mkoani Dodoma.
AWALI, UTARATIBU ULIVYOKUWA
Katika ratiba iliyotolewa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, Julai 9, 2015, Kamati Kuu ya CCM (CC) inakaa kupitia majina yote ya wanachama 38 waliojitokeza kugombea na kuyakata ili kubakisha majina matano yenye sifa kwa mujibu wa mtazamo wa kamati hiyo.
Yalipatikana majina hayo ambayo ni January Yusuf Makamba, Bernard Camillus Membe, Asha–Rose Mtengeti Migiro na Balozi Amina Salum Ali.Julai 10, 2015, Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) kukaa kwa lengo la kupokea hayo majina matano kutoka CC na kuyapigia kura ili yapatikane majina matatu.
Majina matatu yalipatikana ambayo ni John Magufuli (kura 2104 sawa na 87.1%), Asha-Rose Migiro (kura 59 sawa na 2.4%) na Amina Salum Ali (kura 253 sawa na 10.5%).
Akiwa na mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan.
Julai 11, 2015, Mkutano Mkuu wa CCM kukaa kwa ajili ya kuyapigia kura majina matatu ili kupata jina moja kwa ajili ya kupeperusha bendera ya chama hicho dhidi ya wagombea wa upinzani kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa urais utakaofanyika Oktoba 25, mwaka huu.
RATIBA YAPANGUKA
Hata hivyo, katika hali isiyokuwa ya kawaida, ratiba zote hizo hazikwenda sawa baada ya kutokea kwa ugumu uliokuwa nje ya uwezo wa chama. Hadi Julai 11 siku ya Mkutano Mkuu, Nec walikuwa hawajamaliza kikao chao hivyo kuingilia ratiba ambayo si yake.
Matokeo yake, Julai 11 kukawa na vikao viwili, Nec iliyoanza saa nne asubuhi wakiwa wamelala na kiporo walichopewa na CC waliomaliza kikao saa saba usiku na Mkutano Mkuu ambao ulianza saa mbili usiku.
Mabadiliko mengine yaliyojitokeza ni baada ya matokeo ya kumpata mgombea mmoja kushindwa kupatikana hadi jana saa 6:30 usiku ambapo mwenyekiti wa chama hicho aliahirisha kikao mpaka asubuhi ya saa 4:00 tofauti na miaka mingine ya uchaguzi ndani ya chama hicho.
UPINZANI DHAHIRI
Katika hali ambayo haikutarajiwa, kwenye mkutano wa Nec, wakati viongozi wa chama kitaifa wakiingia kwenye Ukumbi wa Dodoma Convention, wajumbe walisimama na kuimba wimbo wa chama huku sehemu ya kumtaja mwenyekiti (Jakaya Kikwete) wao walichomekea jina la Lowassa (Edward) ambaye alikuwa miongoni mwa waliojitokeza kugombea lakini jina lake likakatwa mapema huku kukiwa na malalamiko kwamba, mgombea huyo alionewa.
“Tuna imaaaniii na Lowaaaassa, oyaa! Oyaa! Oyaaa!” baadhi ya wajumbe walisikika wakiimba hivyo.
Baadhi ya wananchi waliokuwa wakifuatilia runingani mkutano huo walisema kulitaja jina la Lowassa kwa wakati huo ilhali alishakatwa ni uasi na upinzani, kwani uwepo wa mwenyekiti ulitaka staha zaidi.
WAJUMBE WA CC KUPINGA
Tukio lingine ambalo lilionesha halijawahi kutokea ni kitendo cha wajumbe watatu kutoka CC kujitokeza hadharani kupinga uamuzi wa wajumbe wengine.
Wajumbe hao ni Emmanuel Nchimbi aliyekuwa msemaji wa wenzake, Sophia Simba na Adam Kimbisa ambao walidai kuwa, katika kikao cha kukata majina matano, kanuni ya chama ya mgombea anayekubalika na wengi ndiye apite, haikuzingatiwa.
Hata hivyo, Nchimbi hakumtaja mgombea anayependwa na wengi japokuwa wengi walimsemea kuwa alimaanisha Edward Lowassa.
LOWASSA GUMZO
Licha ya jina la Lowassa kukatwa mapema katika hatua ya kushindwa kuingia ‘Top 5’, jina lake limeendelea kuwa gumzo kila kona ya nchi, baadhi ya watu wakimzungumzia kwa namna yoyote ile tofauti na wagombea wengine.
Kwenye mitandao ya kijamii, ishu ni Lowassa hadi gazeti hili linakwenda mitamboni. Baadhi ya watu walitupia hivi:
“Hivi kweli Lowassa wamemkata?! Jamani, kweli CC ni kiboko. Hivi sasa itakuaje?
“Hivi ni kwa nini Lowassa amekatwa? Si walisema ndiye atapita kwenye Tano Bora, nini kimetokea? Siasa bwana ni ngumu sana.“Lowassa out! Daa! Kweli CCM ina wenyewe. Lakini naamini hata waliopita wanaweza, mfano Magufuli, anakubalika pia.”
Kwa upande wake Kikwete alisema kuwa kazi aliyopewa na chama chake ya kumpata mgombea anayefaa, ameifanikisha na kinachosubiriwa ni ushindi wa kishindo dhidi ya wapinzani. 

No comments:

Post a Comment

advertise here