Tuesday, 21 July 2015

HIZI NDIO LAWAMA ZA MOURINHO KWA FC PORTO

LAYIII
Iker Casillas amelelewa na Klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa miaka 25, ndani ya kipindi hicho ameichezea Klabu hiyo kwa miaka 16, lakini mambo yakabadilika baadae ambapo mwezi huu alitangaza kuhamia Klabu ya FC Porto ya Ureno kwa mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi.

Mourinho analaumu FC Porto kumsajili Casillas pamoja na mshahara wake?

jose-mourinho-chelsea_e5smuyx0q03h1346wwab0ldj5
Iker Casillas amelelewa na Klabu ya Real Madrid ya Hispania kwa miaka 25, ndani ya kipindi hicho ameichezea Klabu hiyo kwa miaka 16, lakini
mambo yakabadilika baadae ambapo mwezi huu alitangaza kuhamia Klabu ya FC Porto ya Ureno kwa mkataba wa miaka miwili wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi.
Casillas amejiunga na FC Porto na atakuwa analipwa mshahara wa pound milioni 1.7 kwa mwaka.
mou-kicks-iker-514
Hata hivyo kufuatia uhamisho huo kocha wa Chelsea, Jose Mourinho amelaumu uamuzi wa FC Porto kumsajili kipa wa Real Madrid Iker Casillas kwa mkataba wa muda mrefu na wenye maslahi mazuri… Mourinho ambaye aliwahi kuwa kocha wa Real Madrid kati 2010 hadi 2013 hana imani na uwezo wa Casillas kuna wakati aliwahi kumuweka benchi na nafasi yake kumpa Diego Lopez.
Iker19495000
Lakini pia Mourinho alishangazwa na maamuzi mengine ya FC Porto kumsajili kiungo kutokea klabu ya Marsseille ya Ufaransa Giannelli Imbula kwa dau la pound milioni 13.8.
“Siwezi kuamini kama Porto wamelipa pound milioni 13.8 kwa ajili ya Imbula na wanamlipa Casillas mshahara wa ajabu kiasi hiki aina hii ya matumizi inavuruga kabisa utaratibu”>>>> Jose Mourinho.

 


No comments:

Post a Comment

advertise here