LAYIIIII
Maskini! Sexy lady kunako anga la Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, amejikuta akiangua kilio hospitalini kutokana na kile kilichodaiwa ni hasira baada ya kudai kufanyiwa ndivyo sivyo na madaktari, Ijumaa Wikienda lina kisa cha kusikitisha.
Tukio hilo lilijiri wikiendi iliyopita kwenye Hospitali ya Mwananyamala, Dar ambapo mwanadada huyo amekuwa akihudhuria mara kadhaa kwenye kliniki ya kumeza vidonge vya kupunguza makali ya madawa ya kulevya, Methadone.
Chanzo makini cha Ijumaa Wikienda kilieleza kwamba siku ya tukio, Ray C alidamka kuwahi hospitalini hapo kwa lengo la kuchukua dozi yake kisha aendelee na mambo mengine lakini haraka zake ziligonga mwamba baada ya kujikuta akikosa huduma hiyo kufuatia wauguzi kuwa na majukumu mengine.
“Ray C alikuwa anaangua kilio pale Mwanayamala kama mtoto mdogo, nilipomuona nilifikiri kuna tatizo limemtokea kumbe alikuwa amenyimwa dawa na hiyo ilikuwa ni siku ya pili hajanywa kufuatia madaktari kutomhudumia.
“Baada ya kumuona na kunieleza hayo, niliamua kufanya kazi ya ziada kumbembeleza lakini alikuwa na uchungu sana kwani muda wote alikuwa analia, akidai mwili unamuuma kutokana na kutokunywa dawa siku mbili mfululizo,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata ishu hiyo, mwanahabari wetu alimtafuta Ray C ambaye alikiri kufanyiwa ‘umafia’ huo huku msala huo akibaki kumshtakia Mungu kwani alisema kweli siku hiyo alijikuta akilia kwa uchungu kutokana na maumivu makali ambayo yalisababishwa na kutokunywa dawa siku iliyopita.
“Dah kiukweli kuna vitu vinatokea saa nyingine unashindwa kabisa hata kujua kwa nini unafanyiwa hivyo na wakati huohuo kuna hatua tayari unakuwa umeshaanza kupiga kwenye maisha.
“Naumia sana ninapoona mtu anafanya njama za kutaka kunirejesha kwenye maisha mabovu ambayo tayari nimeshaachana nayo, mara nyingine nashindwa kuelewa kwa nini sisi wanawake huwa hatupendani namna hii.
“Kiukweli siku ile nilikuwa kwenye hali mbaya sana kiasi kwamba, nilijikuta nikilia tu maana nilikuwa najilinganisha nilivyokuwa hapo nyuma na leo hii ambapo navutia hadi mbele za watu.
“Ujue mimi hadi naanza kuja hapa kliniki nimepitia kwenye mikono ya watu wengi sana na mara ya kwanza nilikuwa nikihudumiwa bila matatizo, kweli yawezekana mwenyewe nina mapungufu lakini mapungufu yangu hapaswi mtu kuyatumia kuniharibia maisha tena,’ alisema Ray C kwa uchungu huku akiangua kilio, Ijumaa Wikienda likatumia muda wa dakika 20 kumtuliza.
Hata hivyo, Ray C alisema kuwa baadaye walimuhudumia hivyo kwa sasa anaendelea vizuri na dozi ya Methadone.

No comments:
Post a Comment