layiiii
Tunahesabu mwaka wa pili sasa hivi tangu staa wa Muziki ambae ni moja ya matunda mazuri ya THT, Amini Mwinyimkuu aingie
kwenye Headlines baada ya kufunga ndoa.. aliyefunga nae ndoa ni msanii
mwenzake pia, walituahidi album ya pamoja.. vipi huo mpango unaendaje
mpaka sasa?
Amini ana majibu kwenye #255,
amesema mpango uko palepale hakuna kitu kimebadilika na tayari kuna
nyimbo zimerekodiwa na nyingine zinaendelea kupikwa.. time yoyote album
ikikamilika basi tutaanza kuenjoy muziki mzuri wa Wanandoa hao!
Hussein Machozi ndio
kusema anauacha huu muziki? Jamaa amesema zamani alikuwa anacheza sana
mpira wa miguu, baadae akaingia kwenye muziki lakini wamerudi kwenye
meza ya mazungumzo na timu ya Mtibwa Sugar na time yoyote atarudi
uwanjani kwenye soka.
Hussein kasema yeye na muziki bado ni damdam, utamwona kwenye soka na kwenye muziki bado yupo pia !!
Diamond Platnumz
nae kuna kingine kutoka kwake leo, jamaa kasema ameamua kusimamisha
kufanya collabo na wasanii wa nje kwa kuwa mara ya kwanza alizipiga
nyingi ili kutafuta upenyo mzuri Afrika ijue muziki mzuri wa TZ.. YES,
kapiga kazi nyingi na mastaa wengi na hiyo imeuweka muziki wa TZ mahali
pazuri, kwa sasa collabo hizo zitasimama.
Diamond
anasema japo kaamua hivyo lakini kuna foleni ya mastaa ambao nao
wameomba nae collabo mpaka sasa wengine hata hawakumbuki majina yao !!
255 iko hapa mtu wangu, utamsikia Diamond Platnumz, Amini na Hussein Machozi..
No comments:
Post a Comment